test

MADEREVA WANAOZIDISHA ABIRIA WANYOOSHEWA KIDOLE NA POLISI BABATI

 

Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani,  Wilayani Babati,  Mkoani Manyara, limewataka madereva wa magari ya abiria hususani daladala na  hiace kuacha tabia ya kupakiza abiria kupita kiasi kwa tamaa za kujiongezea kipato na kuwataka kuacha mara moja,  kwani ni kosa kwa mujibu wa sheria na kanuni za usalama barabarani pia huweza kusababisha ajali barabarani



Wito huo umetolewa na Sajenti wa Polisi (SGT) Dotto Aloyce kutoka kikosi cha Usalama Barabarani,  Dawati la Elimu Usalama,  Wilaya ya Babati Mkoani Manyara wakati akitoa elimu ya madhara ya chombo cha moto kubeba abiria au mizigo kupitiliza kupitia redio  Revival FM iliyopo Mtaa wa Komoto Kata ya Bagara Halmashauri ya Mji wa Babati


SGT Dotto amesema Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani wilayani hapa linaendelea na operesheni barabarani na   halitakuwa na muhali kwa dereva yeyote atakayekamatwa amezidisha abiria au mzigo  


Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani limekuwa likitumia vyombo vya habari mbalimbali ikiwemo Redio na TV kutoa elimu za usalama barabarani ili kuzuia na kupunguza ajali

MADEREVA WANAOZIDISHA ABIRIA WANYOOSHEWA KIDOLE NA POLISI BABATI MADEREVA WANAOZIDISHA ABIRIA WANYOOSHEWA KIDOLE NA POLISI BABATI Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on February 03, 2026 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.