test

TPF -NET MANYARA KUADHIMISHA SIKU WANAWAKE KWA KUWATEMBELEA WENYE UHITAKI MAALUMU

 Sikuya wanawake Duniani Machi 8 2026 Mrakibu Mwandamizi wa Polisi kutoka Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake (TPF-Net) Mkoani hapa Januari 30, 2026 amefanya kikao kazi na maafisa, wakaguzi na askari wa kike kwa lengo la kukumbushana wajibu wa  kazi za kulinda raia na mali zao pamoja na  kujadili namna bora ya kushiriki siku ya Mwanamke duniani ambayo huadhimishwa  March 8 kila mwaka



Katika kikao hicho  hicho kilifanyika  ukumbi wa bwalo la maafisa wa Polisi Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara pamoja na mambo mengine, TPF-net Manyara mwaka huu,  wameafikiana kuaadhimisha siku ya Mwanamke Duniani kwa kuwatembelea na kutoa misaada kwa  watu wenye mahitaji maalum, kutoa elimu mbalimbali ikiwemo elimu ya Sheria, ndoa, mambo ya ujasiriamalia, protokali kwa askari na jamii, kuwapatia zawadi askari wa kike waliofanya vizuri ili kuwaongezea motisha katika utendaji kazi


Kila mwaka Machi 08 Jeshi la Polisi huungana na Dunia kuadhimisha siku ya Mwanamke duniani ikiwa na lengo la kutambua mchango na uwezo wa mwanamke katika kudumisha usalama na amani katika jamii

TPF -NET MANYARA KUADHIMISHA SIKU WANAWAKE KWA KUWATEMBELEA WENYE UHITAKI MAALUMU TPF -NET MANYARA KUADHIMISHA SIKU WANAWAKE KWA KUWATEMBELEA WENYE UHITAKI MAALUMU Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on February 01, 2026 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.