test

TAASISI YA TEKNOLOJIA DAR ES SALAAM ( DIT ) YASAINI MAKUBALIANO YA KUENDESHA MAFUNZO YA PAMOJA NA TAASISI YA CHONGQING YA NCHINI CHINA

 TAASISI ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), imesaini makubalino ya kuendesha mafunzo ya pamoja na Taasisi ya Chongqing Vocation Institute of Engineering (CQVIE) ya China ambapo wanafunzi wa kitanzania watanufaika kwa kupata shahada na stashahada katika taasisi hiyo.

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mh.Profesa Adolf Mkenda amesema wanafunzi wa kitanzania watapata shahada ya Uhandisi Ujenzi kutoka Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) na stashahada ya Ujenzi kutoka Taasisi ya Chongqing Vocational Institute of Engineering (CQVIE) ya China.

Profesa Mkenda amesema programu hiyo inaanza mwaka huu ambayo itafanya mambo makubwa matatu ikiwemo kubadilishana wanafunzi, kubadilishana walimu pamoja na kuwaunganisha wanafunzi na viwanda kwa lengo la kujifunza zaidi.

Amesema DIT itasajili wanafunzi ambao watasoma katika taasisi hiyo kwa mwaka wa kwanza, mwaka wa pili na wa tatu watasoma mafunzo ya ufundi stadi katika chuo cha  CQVIE  China ambapo watatunikiwa stashahada ya  Ujenzi na mwaka wa nne watarudi DIT ambapo watatunikiwa shahada ya Uhandisi Ujenzi.

Pia amesema kutakuwa na kipengele cha kubadilishana wakufunzi wa China na Watanzania ambao wataenda China kuangalia namna ambavyo wenzeo wanavyofundisha wanafunzi wao kubadilishana mawazo lakini pia DIT itapata wakufunzi toka China ambao watakuja kufundisha madarasani kwa pamoja kwa lengo la kuboresha.

Prof. Mkenda amesema  programu hiyo itasaidia kuunganisha vizuri zaidi wanafunzi wanaoenda kusoma na maeneo ya kazi, akatolea mfano Kampuni kubwa ya nchini China inayofanya kazi za  Ujenzi hapa nchini ijulikanayo kama Group 6 ambayo itashirikiana na DIT hasa kwa wanafunzi wanaotarajiwa kwenda kusoma masomo ya Uhandisi Ujenzi kupata fursa ya kwenda kujifunza kwa vitendo lakini kupata ajira watakapo hitimu.

Kwa maelezo ya Prof. Mkenda, programu hiyo itaanza na wanafunzi takriban 30 lakini jitihada zitaendelea kufanyika kuhakikisha kuwa idadi ya wanafunzi inaongezeka kwa kasi ili kuweza kupeleka wanafunzi wengi zaidi China.


Alisema juhudi hizo ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa kila mara anasisitiza elimu iandae wanafunzi ambao wataweza kujiajiri kirahisi hivyo aina hiyo ya mafunzo itaongeza uwezekano wa wanafunzi wanaomaliza kupata ajira ya moja kwa moja ndani na nje ya Tanzania .

Kwa upande wake mwenyekiti wa Baraza la DIT, Dk Richard Masika alishukuru kwa makubaliano hayo baina Taasisi hizo na kuahidi watasimamia programu hiyo kwa ufanisi mkubwa ili kuhakikisha inakuwa endelevu ili kufungua milango mingine ya ushirikiano zaidi.

TAASISI YA TEKNOLOJIA DAR ES SALAAM ( DIT ) YASAINI MAKUBALIANO YA KUENDESHA MAFUNZO YA PAMOJA NA TAASISI YA CHONGQING YA NCHINI CHINA TAASISI YA TEKNOLOJIA DAR ES SALAAM ( DIT ) YASAINI MAKUBALIANO YA KUENDESHA MAFUNZO YA PAMOJA NA TAASISI YA CHONGQING YA NCHINI CHINA  Reviewed by Adery Masta on December 01, 2022 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.