Aliyeunguliwa na nyumba akabidhiwa msaada wa uliochangishwa na wadau pamoja na wananchi
Husna Hassan aliyeunguliwa na nyumba miezi Miwili iliyopita Leo Mei 11.2025 Amekabidhwa Msaada wa Bati na Mbao zilizochangiwa na wadau mbali mbali Mjini Babati.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo katibu wa mbunge wa Babati mjini bw.Abrima Hussein, amesema kuwa jumla ya Fedhea zilizochangiwa ni Tsh 970,000 ambazo zimefanikisha ununuzi wa Bati 38 na Mbao 15.
Aidha wananchi wa Mtaa wa maisaka kati wamechangia Tsh 150,000 ambazo zimekabidhiwa Kwa bi.Husna kupitia Kwa Mwenyekiti wa Mtaa huo.
Hata hivyo bi Husna ameshukuru wadau na wananchi Kwa mchango huo nakuomba wananchi kuendelea kumchangia kwani Bado anauhitaji mkubwa kwani kuungua Kwa nyumba yake kumeathiri maisha yake kutokana na kuunguliwa na mali zote zilizokuwa ndani .
