Kada wa Chama cha Mapinduzi CCM kutokea Babati Mkoani Manyara, Aminatha Shamghe ambaye pia ni mwandaaji wa shindano la kusaka walimbwende la Miss Tanzanite, ameonesha nia ya kugombea ubunge katika Jimbo la Babati Mjini.
Akizungumza juu ya kutia nia kwake Aminatha amesema ana nia ya dhati ya kuwapatia wananchi maendeleo yatakayoendana na ukuaji wa kasi ya maendeleo ya Dunia ikiwemo ukuaji wa Teknolojia na Maisha bora.
Ili kutimiza hayo, amesema atahakikisha anawanunulia wananchi wa Jimbo hilo simu janja (Smartphone) ili kuishi kidijitali, pamoja na kutoa usafiri wa magari kwa wajumbe jimboni humo.
AMINATHA ATIA NIA UBUNGE, AAHIDI KUMNUNULIA SMARTPHONE KILA MWANANCHI
Reviewed by VISION MEDIATZBLOG
on
May 31, 2025
Rating:

No comments: