Baadhi ya washindi pesa taslimu katika droo ya saba ya Kampeni ya Ndinga la Kishua katika picha ya pamoja.
Meneja wa Wateja Maalum Tigo Pesa Mary Rutta akimkabidhi zawadi ya Vifaa vya Hisense ambavyo ni SMART TV , Sub woofer , Micro wave na Friji Mmoja kati ya Washindi wawili wa Droo ya wiki ya Saba , kulia ni Afisa masoko wa kampuni ya HISENSE Bwn.Joseph Mavura
Na Mwandishi Wetu.
Dar es Salaam Januari , 13 , 2023: Kampuni ya mtandao wa simu za mkononi ya Tigo, leo imewakabidhi zawadi zao washindi wa droo ya saba ya Kampeni ya Ndinga la Kishua inayochezeshwa kwa watumiaji wa miamala ya Tigo Pesa.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Meneja wa Wateja Maalum wa Tigo Pesa, Bi. Mary Rutta amesema kampuni hiyo inafuraha kubwa kuendelea kuwazawadia wateja wake zawadi hizo na kuwataka wengine kuendelea kufanya miamala ya Tigo Pesa ili nao kujishindia zawadi mbalimbali kama vile pesa taslimu, vifaa vya Hisense au Ndinga jipya kabisa la Kishua aina ya Rush. Meneja huyo aliendelea kusema;
“Leo tuko kwenye tukio lingine la kutoa zawadi kwa washindi wetu wa droo ya saba katika kampeni ya Ndinga la Kishua , tumebakiza droo moja tu ya wiki kumaliza kampeni yetu na pia tumebakiza droo kubwa ya kushinda milioni 10 na Milioni 20 pamoja na gari jipya kabisa aina ya TOYOTA RUSH , Nawasihi watja wetu kufanya miamala mingi kwa kipindi hiki kifupi kilichobakia maana mwisho wa miamala kuhesabiwa ni Jumapili ya Tarehe 15 mwezi huu , Nasisitiza Fanya miamala kwa kutumia Tigo Pesa kutuma pesa mitandao mingine, Tigo kwenda Tigo, kulipa bili, kutuma na kupokea pesa kutoka benki, kutuma na kupokea pesa kutoka nje ya nchini, kukopa fedha kupitia huduma ya Bustisha au Nivushe, kufanya malipo serikali ili kujiweka katika nafasi ya kujishindia zawadi hizo" Alimalizia
Naye Afisa masoko wa kampuni ya HISENSE Bwn.Joseph Mavura amesema kuwa kampuni ya Hisense
Inatoa punguzo la 20% katika maduka yao yote na huduma ya kusafirishiwa bidhaa utakazo nunua hadi nyumbani kwako bure (FREEE DELIVERY), hii ni kwa wateja wote watakao nunua bidhaa kutoka hisense na kulipia kwa njia ya Tigo pesa, pia tunaendelea kutoa vifaa vya Hisense kwa washindi wawili kila wiki , Alimalizia.
JINSI YA KUIBUKA MSHINDI PROMOSHENI YA NDINGA LA KISHUA YA TIGO
Reviewed by Adery Masta
on
January 13, 2023
Rating:
No comments: