test

TIGO WATOA ZAWADI YA GARI NA MAMILIONI YA PESA KWA WATANZANIA

 





FAINALI ya shindano la Ndinga la Kishua, imemalizika jana ambapo mkazi wa mkoa wa Kahama, Samson Daniel Samson ameibuka kidedea na kujishindia gari aina ya Toyota Rush, huku washindi wengine wakibeba fedha taslim na vifaa vya nyumbani kama walivyobainishwa kwenye picha hapo juu.

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi hao, Meneja wa Wateja Maalumu wa Tigo Pesa, Mary Rutta alisema wamekabidhi zawadi kwa washindi wa droo ya nane na ya mwisho. Alisema pia wametoa vifaa vya kisasa kutoka Hisense kwa washindi vikiwemo microwave, spika za muziki, friji, tv na zinginezo.

Kampeni hii imefikia tamati na leo tumempata mshindi wa gari mpya aina ya Toyota Rush ambayo haijatumika kabisa, Pia katika droo ya nane tumepata washindi wa fedha taslimu ambao wamekabidhiwa zawadi zao, hii itasaidia kuanza mwaka vizuri kwani kila mmoja anatambua ugumu wa mwanzo wa mwaka mpya. “Washindi walipatikana kwa njia ya za kulipa bili, mikopo ya bustisha, malipo ya kiserikali, kutuma na kupokea pesa kutoka benki kwa njia ya Tigo Pesa,” alisema Mary.

Naye Ofisa Masoko wa Kampuni ya Hisense, Joseph Mavura alisema kuwa kampuni hiyo ilikuwa ikitoa punguzo la 20% katika maduka yao yote na huduma ya kusafirishiwa bidhaa hadi nyumbani bure katika kipindi chote cha shindano hilo.

“Mpaka sasa tumeshapata washindi wa vifaa vya Hisense ambavyo ni tv, microwave, friji na spika za muziki, napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru Watanzania kuendelea kufanya miamala,” alisema.
TIGO WATOA ZAWADI YA GARI NA MAMILIONI YA PESA KWA WATANZANIA TIGO WATOA ZAWADI YA GARI NA MAMILIONI YA PESA KWA WATANZANIA Reviewed by Adery Masta on January 19, 2023 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.