test

BIHIMBA MPAYA ATOA VIFAA VYA MICHEZO S/M MISITU - UKONGA DAR ES SALAAM

 



Bwn. Bihimba Mpaya ( katikati ) akikabidhi Vifaa vya Michezo kwa Viongozi wa Michezo Shule ya Msingi Misitu , Pembeni yake ( aliyevaa Kofia ) ni Bwn . Hussein Lugome.


Baadhi ya Wanafunzi Shule ya Msingi Misitu , wakifurahia ujio wa 
Bwn. Bihimba Mpaya

Na Mwandishi Wetu

Mwanaharakati Huru hapa nchini Bwn. Bihimba Nassor Mpaya Mkazi wa Kivule - Ukonga Jijini Dar Es Salaam Leo Aprili 28 , 2023 ametoa Vifaa vya Michezo katika Shule ya Msingi Misitu iliyopo Kivule Ukonga Jijini Dar Es Salaam , Ikiwa ni sehemu ya kuiunga mkono serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuboresha na kukuza vipaji vya michezo kwa wanafunzi hasa wa Shule za Misingi .

Akizungumza baada ya kukabidhi Vifaa hivyo ambavyo ni Mipira Miwili na Jezi za Michezo Bihimba amesema kuwa ataendelea kuisaidia serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mambo tofauti tofauti ili kuleta ustawi na hamasa kwa jamii katika nyanja mbalimbali .

" Leo nimefika hapa Shule ya Msingi Misitu kwa kuitikia wito wa Mwalimu Mkuu , Namimi baada ya kuambiwa kwamba mna upungufu wa Vifaa vya Michezo nikaona nifike kuwapatia vifaa hivyo kama ambavyo nimekuwa nikifanya katika shule nyingine , Lengo ni kuleta Ustawi katika jamii na kuwatia moyo maana michezo ni sehemu ya Masomo yenu " Alisema Bihimba

Naye Bakhari Ally , Mwenyekiti wa Kamati ya Shule ya Msingi Misitu amempongeza Bwn. Bihimba kwa Moyo wake wa kipekee wa kutoa katika Jamii , na kuwasihi wanafunzi waweze kujitahidi katika Masomo na Michezo maana jamii inawaunga mkono.

BIHIMBA MPAYA ATOA VIFAA VYA MICHEZO S/M MISITU - UKONGA DAR ES SALAAM BIHIMBA MPAYA ATOA VIFAA VYA MICHEZO S/M MISITU - UKONGA DAR ES SALAAM Reviewed by Adery Masta on April 28, 2023 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.