Na Mwandishi Wetu.
Kampuni ya Mawasiliano nchini, Tigo imeongeza wigo wa soko la bidhaa zake kwa kuwafikia wadau wa sekta ya Utalii wanaoshiriki kwenye maonyesho ya Karibu Kill Fair 2023, mjini Arusha.
Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini, Erick Sostenes amewakaribisha watu mbalimbali wakiwemo wadau wa Utalii kutembelea banda lao namba 28 ndani ya maonyesho hayo ya msimu wa nne mwaka huu huku huduma za simu, mawasiliano ya intaneti na zingine zikiendelea kutolewa hapo.
"Karibuni kwenye banda letu la tigo namba 28 ndani ya Kili Fair 2023, kwa huduma za bidhaa za simu, tigopesa, intaneti kwa gharama nafuu." Amesema Sostenes.
Kwa upande wake mmoja wa wateja waliofika kwenye banda lao hilo, Jacobo Sima mkazi wa Arusha, amefurahia huduma za Tigo ikiwemo kununua simu ya bei rahisi na kwa mkopo.
"Nimefika hapa sikuwa na pesa taslimu lakini kupitia mkopo nimeweza kupata simu yangu.
Imeniwezesha kufurahia bidhaa za Tigo " amesema Jacobo
Aidha, Tigo imeendelea kutoa huduma zake za mawasiliano ikiwemo kwa wadau wa ndani na nje wanaofika kwenye maonesho hayo ya Utalii.
No comments: