test

MAMA MFANYABIASHARA YA NGUO ASHINDA MILIONI 1 KAMPENI YA " TIGO CHA WOTE" , WASHINDI TAKRIBANI 11200 NDANI YA WIKI TANO.

 Na Mwandishi Wetu. 

Bi. Indu Bakari Mkundi Mfanyabiashara ya Nguo Mkazi wa Goba Jijini Dar Es Salaam ni miongoni mwa washindi wa Milioni Moja,  Kampeni ya Tigo CHA WOTE wiki ya tano ambapo hadi sasa Tigo wameshatoa Fedha Taslim na zawadi mbalimbali kwa Washindi Takribani 11200  Nchi Nzima tangu kampeni hii izinduliwe. 





Akizungumza Leo Julai 21, 2023. Wakati wa Kuwakabidhi Mfano wa Hundi Baadhi ya Washindi wa Milioni Moja Moja wiki ya tano waliobahatika kufika Tigo Makao Makuu, Balozi wa Kampeni ya CHA WOTE Mtangazaji MILLARD AYO amesema kuwa hadi sasa ikiwa ni wiki tano tu tangu Kampeni iyo izinduliwe wameshapatikana washindi Takribani 11200  kutoka maeneo mbalimbali nchini .

" Leo tunayo furaha kubwa kuwa na baadhi ya washindi wa Wiki ya tano wa Kampeni  ya TIGO CHA WOTE ambao hawa ni washindi wa Milioni Moja Moja kila mmoja, Lakini niwakumbushe Watanzania kwamba kila siku CHA WOTE inatoa zawadi ikiwemo pesa taslimu hadi Milioni Moja kwa washindi 320 kila siku , kuibuka mshindi ni rahisi tu unachotakiwa ni kufanya miamala na Tigo Pesa kama Kutumia Lipa Kwa Simu , Kununua Vifurushi , Kulipia Bili kwa Tigo Pesa , n.k kwa kufanya ivyo nawewe siku si nyingi utakua miongoni mwa Washindi wa Kampeni hii ya CHA WOTE , haijalishi hata kama ukinunua laini leo na ukaanza kutumia huduma za Tigo Pesa moja kwa moja unakua katika nafasi ya kushinda ".  " Alisema MILLARD AYO

Naye Mmoja wa Washindi wa Milioni Moja,  Bi. Indu Bakari Mkundi mfanyabiashara ya Nguo za wanawake  kutoka GOBA Dar Es Salaam amesema kuwa ana furaha kubwa kuibuka mshindi wa Kampeni hii na hakutegemea kama hata Watanzania wenye kipato cha kawaida wanaweza kushinda

" Kwakweli nikiri nimefurahi sana jamani , Mimi Nafanya biashara ya Nguo ambapo nanunua Nguo Kariakoo na kuzisafirisha mikoa ya Kusini huko  na huwa nafanya miamala mbalimbali kama kulipia bili , na kununua Vifurushi vya SMS na Muda wa Maongezi nafikiri ivyo ndo vimenifanya nkawa mshindi , kwakweli hakika hiii ni CHA WOTE maana kumbe inawezekana kila mtu akawa mshindi hata sisi wenye kipato cha kawaida kwa maana mimi mtaji wa biashara yangu ni laki tano tu  , katika maisha yangu Sikumbuki kama nilishawahi kushinda chochote,  hii milioni moja inaenda kubadilisha Biashara Yangu kwa maana naenda kuongezea mtaji kutoka Laki tano hadi Milioni tano sasa kwakweli TIGO CHA WOTE imeni "Boost " " Alisema Bi. Indu.

Washindi wengine waliokabidhiwa Hundi zao Makao makuu ya Tigo Leo hii ni Levison Blassio mfanyabiashara wa Spare za Pikipiki na Maziwa Mkazi wa Bariadi na Grace Katoto Mkazi wa Kitunda Jijini Dar Es Salaam.

MAMA MFANYABIASHARA YA NGUO ASHINDA MILIONI 1 KAMPENI YA " TIGO CHA WOTE" , WASHINDI TAKRIBANI 11200 NDANI YA WIKI TANO. MAMA MFANYABIASHARA YA NGUO ASHINDA  MILIONI 1 KAMPENI YA " TIGO CHA WOTE" , WASHINDI TAKRIBANI 11200 NDANI YA WIKI TANO. Reviewed by Adery Masta on July 28, 2023 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.