test

MSHINDI WA MILIONI TANO YA " CHA WOTE " KUTOKA ZANZIBAR

WAWEZA KUTAZAMA VIDEO HAPA

 Ikiwa ni Takribani siku Kadhaa Tangu Kampuni ya Mawasiliano ya Tigo Zantel izindue Kampeni yake CHA WOTE yenye lengo la kuwasaidia Wataja wao kutimiza Malengo  waliojiwekea ndani ya Mwaka huu, Angelina Albat amekuwa mshindi wa Mwanzo kutoka Visiwani Zanzibar kushinda Shilingi milioni Tano katika kampeni hiyo ya CHA WOTE.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Darajani Mjini Unguja wakati wa sherehe fupi ya kukabidhia Mfano wa Hundi ya Ushindi wa Kampeni hiyo ya CHA WOTE, Angelina Albet amesema kuwa, ana furaha kubwa ya kuibuka mshindi wa Kampeni hii na hakutegemea kama hata Watanzania wenye kipato cha kawaida wanaweza kushinda.


Angelina ambae ni Mfanya biashaa amesema kuwa, fedha hizo anatarajia kuzitumia katika kukuza biashara ambayo anaifanya pamoja na kutumia katika mahitaji yake ya kila siku.


"Kwakweli nikiri nimefurahi sana baada ya kuibuka Mshindi wa Shilingi milion Tano, Fedha hizi nitazitumia katika kuendeleza biashara yangu ambayo ninaifanya, huwa nafanya miamala mbalimbali kama kulipia bili , na kununua Vifurushi vya SMS na Muda wa Maongezi nafikiri ivyo ndo vimenifanya nkawa mshindi," ameeleza.


"Inawezekana mtu kushinda na Washindi huwa hawapangwi hivyo natoa wito kwa Watu kuendelea kufanya Miamala na kununua Bidha kwa Tigo Pesa wanaweza kushinda kama nilivyoshinda Mimi," aliongeza Angelina Albat.


Kwa Upande wake Meneja wa Mauzo Tigo Zantel Zanzibar Saleh Abdul Saleh amesema kuwa Kampeni hiyo ya inawawezesha Watanzania zaidi 320 kila siku kushinda zawadi mbalimbali kama vifurushi vya Dakika na MB pamoja na fedha taslimu Milion Moja hadi milion Tano kwa kufanya miamala tu kupitia Tigopesa.


"Leo hapa tunafuraha ya kumkabidhi Mfano wa Hundi Mshindi wetu wa kwanza wa Shilingi Milion Tano kutoka Zanzibar Tangu kuanza kwa kampen hii ya CHA WOTE ambapo watanzania mbalimbali wanajishindia zawadi tofauti tofauti kila siku," alieleza.


Amewakumbusha Watanzania kuendelea kufanya miamala na Tigopesa ili kuibuka Washindi na kutimiza Malengo yao waliojiwekea ndan ya Mwaka huu.


"Niwakumbushe Watanzania kwamba, kila siku tunatoa zawadi za pesa taslimu hadi milioni Moja kwa washindi 320 sasa wanatakiwa kuendelea kutumia Lipa kwa Simu, kununua vifurushi, kulipia Bii kwa Tigo Pesa ili kuwa miongoni mwa Washindi wa Kampeni hii ya CHA WOTE," alisema.


Alifafanua kuwa, kwa Kila Siku kuna Wateja zaidi ya Elfu 18 ambao wanashinda shilingi Elfu 5, Wateja Elfu 9 wanashinda Shilingi Elfu 10, Wateja Elfu 1800 wanashinda Elfu 50,000 na Wateja Wanashinda Milioni Moja pamoja na Mteja Mmoja anaeshinda Shilingi Milion Tano kwa Mwezi.

MSHINDI WA MILIONI TANO YA " CHA WOTE " KUTOKA ZANZIBAR MSHINDI WA MILIONI TANO YA " CHA WOTE " KUTOKA ZANZIBAR Reviewed by Adery Masta on July 27, 2023 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.