test

BASHUNGWA ATAKA UBUNIFU WIZARA YA YA UJENZI

 Waziri wa Ujenzi,  Innocent Bashungwa amewataka  watendaji na wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi kuongeza ubunifu na uadilifu ili kufikia malengo ya Serikali  katika Sekta ya ukuaji na uendelezaji wa miundombinu nchini.


Akizungumza mara baada ya kuwasili Wizarani hapo Waziri Bashungwa amesema kuwa nia ya Serikali ni kuhakikisha miundombinu ya barabara, madaraja, majengo na wataalam katika sekta hiyo wanaongezeka kwa wingi na ubora ili kuleta tija kwa Taifa.


“Siri ya mafanikio yoyote katika utendaji ni ushirikiano, hivyo naomba tushirikiane, tufanye kazi kwa weledi na ubunifu ili kujenga Taifa hili”, amesema Bashungwa


Aidha, Waziri Bashungwa amewataka wafanyakazi wote kufanya kazi kwa malengo yanayopimika ili kuiwezesha Serikali kufikia malengo na kuleta tija kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.


Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhandisi Godfrey Kasekenya, amemkaribisha Waziri Bashungwa Wizarani hapo na kumhakikishia kuwa Wizara hiyo ina timu yenye watu weledi watakaomsaidia kutimiza malengo ya Serikali katika kuliletea Taifa maendeleo katika sekta ya muindombinu.


BASHUNGWA ATAKA UBUNIFU WIZARA YA YA UJENZI BASHUNGWA ATAKA UBUNIFU WIZARA YA  YA UJENZI Reviewed by VISIONMEDIA on September 04, 2023 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.