Taasisi ya Teknolojia Dar Es Salaam inashiriki Maonesho ya Kongamano la 20 ya Wahandisi Nchini ( 20th Annual Engineers Day 2023 ) yanayoendelea katika Viwanja vya Mlimani City Jijini Dar Es Salaam.
Akizungumza mapema Leo hii Septemba , 14 , 2023 Mkuu wa Kitengo Cha Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma - DIT Bwn. Amani Kakana amesema Taasisi hiyo inayo furaha kubwa kushiriki Maonesho haya na inajivunia kuwa Takribani 30% - 40% ya Washiriki wa Maonesho haya ni Wahitimu wa DIT " Naomba niwakaribishe wadau wote katika banda letu la DIT ambapo katika Kipindi hiki cha Maonesho tumewaandalia Mambo mengi mazuri ya Kiteknolojia ambayo mtakutana nayo, Na baadhi ya Mambo hayo ni Gari inayotumia Gesi ambayo inaeleza namna mfumo wa gas unavyofungwa kwenye gari na faida zake katika kuokoa pesa, lakini pia tunayo bajaji ya Umeme pamoja na Bunifu nyingi zinazofanywa na Wanafunzi wetu , Karibuni sana Bandani kwetu mjionee " alimalizia Bwn. Kakana
DIT WAJA KIVINGINE MAONESHO YA KONGAMANO LA 20 LA WAHANDISI NCHINI
Reviewed by Adery Masta
on
September 14, 2023
Rating:
No comments: