Mfanyabiashara na Mkazi wa Mjini Mwanza Mhandisi Peter Mbawala ameipongeza huduma nzuri inayotolewa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni BRELA inayotolewa katika Maonyesho ya 6 ya Kimataifa na Teknolojia ya Madini Mjini Geita.
Mhandisi Mbawala amesema anafurahia huduma inayotolewa la BRELA kwani wanatoa kwa haraka na Kwa uhakika zaidi.
Kupitia Maonyesho hayo amewataka Wafanyabiasha mbalimbali kuweza kujitokeza ili kwenda kupata huduma itolewayo na BRELA ili kuhakikisha kufanya Biashara Kwa furaha na amani.
" Mimi Mhandisi Peter Mbawala nimetokea Mwanza, nimekuja BRELA kufuatilia na kupokea cheti Cha usajili wa jina la Biashara, nimepata kwa urahisi kabisa , na sasa naendelea kutembelea mabanda Mengine
mbalimbali ili kujionea mambo Mengine mazuri" amesema Mbawala.
Naye Afisa wa Wakala wa Usajili wa Biashara na leseni ( BRELA ) Vincent Nyanje amewataka wananchi na Wafanyakazi mbalimbali kuweza kutembelea banda lao la BRELA ili kuweza kujifunza huduma mbalimbali zinazotolewa na BRELA.
No comments: