Mkuu wa mkoa wa Manyara Mhe. Qeen Cuthbert Sendiga Mapema hii leo ameungana na wakazi wa mji wa Babati kushiriki zoezi la usafi wa mazingira katika eneo la soko kuu Babati mjini.
Mhe. Queen amewataka wananchi kujijengea tabia ya kufanya usafi wa mazingira mara kwa mara ikiwemo katika miundombinu ya maji taka (mitaro) katika maeneo yao ikiwa ni sehemu ya kuchukua tahadhari ya kukabiliana na maafa kufuatia kuwepo uwezekano wa ujio wa mvua kubwa za Elnino mkoani Manyara.
Uwajibikaji rafiki wa maendeleo🇹🇿
#ManyaraKunawaka🔥
RC MANYARA AJUMUIKA NA WANA NCHI KUFANYA USAFI WA MAZINGIRA
Reviewed by VISIONMEDIA
on
September 09, 2023
Rating:
No comments: