Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Cuthbert Sendiga, amefanya kikao maalum na Wazee wa Mila, Viongozi wa Dini na Wazee Mashuhuri.
Lengo ikiwa ni kujadili masuala mbalimbali ya Maendeleo na kuwajuza Juu ya maandalizi ya Kilele cha Mbio za Mwenge Wa Uhuru 2023 pamoja na kuwaalika kushiriki maadhimisho hayo.
Pamoja na mambo mengine Mhe. RC amewaomba Viongozi hao kusimamia suala la malezi na maadili ya Vijana. Katika kikao hicho Mkuu wa Mkoa alipata wasaa wa kusikiliza kero, kupokea ushauri na maoni ya viongozi hao ambao walizungumzia masuala mbalimbali ya Kijamii.
Akihitimisha kikao hicho, Mkuu wa Mkoa amewashukuru wazee na Viongozi wote wa Dini kwa ushirikiano waliompa tangu amehamia katika Mkoa wa Manyara na ameahidi kuendelea kushirikiana nao kila wakati. Aidha, amemuelekeza Katibu Tawala wa Mkoa kupanga ratiba ya kuwa na kikao cha aina hiyo mara mbili 2 kwa mwaka.
No comments: