MAMLAKA ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya nchi imesema itaendelea kufanya operesheni ya kuwakamata na kuwachukulia hatua za kisheria watu wanaolima bangi katika mikoa yote.
Hayo yameelezwa leo na Kamishna jenerali Aretas Lyimo wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema bangi bado ni tatizo kubwa katika Nchi na inalimwa mikoa yote.
Kamishna Lyimo amesema wamefanya udhibiti wa dawa za viwandani ikiwemo Heroine na Cocaine ndio watumiaji sasa wamehamia kwa kiwango kikubwa kwenye kutumia bangi.
Ili kufanikisha zoezi hilo amesema wataanza kushirikiana na Mamlaka za maji na Mabonde ya maji kwa kuwa bangi watu wengi wanailima kwenye vyanzo vya maji.
Amewaomba wazazi kushirikiana na Mamlaka hiyo ili kutokomeza kilimo cha bangi na matumizi yake.
#Dawa za kulevya
No comments: