test

RPC, MANYARA ATAHADHARISHA WAVUNJIFU AMANI .


 Jeshi la polisi mkoani Manyara limesema mwananchi yeyote atakayejihusisha na vitendo vya uvunjifu wa amani pamoja na uhalifu wakati wa kiliele Cha mbio za mwenge 2023 atachukuliwa hatua Kali za kisheria.


Hayo yamebainishwa na kamanda wa  polisi mkoani humo ACP George Katabazi wakati akizungumza na Vision Media ofisini kwake mapema hii leo kuelekea ujio wa mwenge wa Uhuru pamoja na kiliele chake Katika mkoa huo.


Kamanda Katabazi amesema Jeshi limejipanga kikamilifu kuhakikisha linaimarisha ulinzi zaidi kuanzia kwenye mapokezi ya mwenge huo yatakayofanyika octoba 7 mwaka huu Katika wilaya ya kiteto mpaka Siku utakapozimwa octoba 14 Katika mji wa Babati Mkoani Manyara.


Ameongeza kuwa kwa yeyote ambaye atajaribu kupima uwezo wa Jeshi hilo kwa kufanya vitendo vya uhalifu pamoja na kuharibu amani na usalama wa Mkoa huo atakutana na mkono wa Sheria kwa polisi mkoa wa Manyara wamejipanga kukabiliana na vitendo hivyo.


Ikumbukwe kwamba Mwenge wa uhuru unatarajiwa kuanza mbio zake Mkoani manyara octoba 7 na kufikia kiliele octoba 14 kwa kuzimwa Katika uwanja wa kwaraa uliopo Mjini babati ukienda sambamba na kumbukizi ya kifo Cha Baba wa Taifa Hayati mwalimu Julius kambarage Nyerere.

RPC, MANYARA ATAHADHARISHA WAVUNJIFU AMANI . RPC, MANYARA  ATAHADHARISHA WAVUNJIFU AMANI . Reviewed by VISIONMEDIA on October 06, 2023 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.