Na Mary Margwe, Geita
MKUU wa kitengo cha utafiti ,masoko na Maendeleo kutoka kampuni ya Orbit Securities limited Fortius Rutabingwa amewataka wachimbaji kuchangamkia hisa kwenye Soko la mitaji ili kuweza kutimiza ndoto zao.
Rutabingwa ameyasema hayo Jana wakati akizungumza na waandishi wa habari walipotembelea banda la Kampuni ya Orbit Security kwenye Maonyesho ya sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini Geita 2023.
Amesema Kampuni ya Orbit security ni kampuni ya wakala wa Soko la Hisa ambapo kwa mara ya kwanza wameshiriki Maonyesho hayo na hivyo kuwataka wachimbaji wadogo kuhakikisha wanachangamkia fursa ya uchukuaji wa Hisa kwenye Soko la mitaji ili kuweza kuirahisishia kufikia malengo waliyokusudia.
Aidha Rutabingwa amefafanua kuwa kuweka pesa kwenye eneo soko la mitaji la Hisa na kwenye migodi ya Madini kunahitaji Uwekezaji wa mtaji mkubwa, hivyo wananchi wanaweza kuungana nanhata kwa mtu mmoja mmoja Orbit inaweza kuwashika mkono.
" Lengo la sisi kuja hapa kwenye Maonyesho haya ni kuwaelimisha wananchi ili kutambua umuhimu wa hisa na hapa ni muhimu wananchi wakaungauna na hata kama mtu akiwa mmoja basi Orbit wanaweza kukushika mkono" amefafanua Rutabingwa.
Aidha awali mwitikio ulikuwa sio mkubwa sana kutokana na maeneo hayo kutojua na kukosa ufahamu wa kutosha kuhusu fursa zilizopo kwenye soko la mitaji, hivyo ushiriki wao kwenye Maonyesho hayo yamewasaidia sana kutoa elimu hii kwa mapana zaidi.
"Awali mwitikio ulikuwa sio mkubwa sana kutokana na maeneo hayo kutojua na kukosa ufahamu wa kutosha kuhusu fursa zilizopo kwenye soko la mitaji, hivyo ushiriki wetu kwenye Maonyesho haya yametusaidia sana kutoa elimu hii Kwa mapana zaidi " amesema Rutabingwa.
Ameongeza kuwa kupitia Soko la mitaji wananchi kama wanakuwa wameshajiunga na kuwa na sifa wao wataendelea kuwapa mitaji ya muda mrefu kwani tayari watakuwa wameshakuwa na uwazi kwenye shughuli zao .
Mkuu huyo wa kitengo cha utafiti Amesema sehemu nyingine ambayo wao wamekuwa wakiisisitiza nikuhusu wa chimbaji wadogo au wa kati ambao wanandoto za kukuza mitaji yao na kwamba badala ya kutegemea kupata mitaji kwenye mabanki lakini pia nifursa zipo kwenye soko la mitaji
Pia amefafanua uwekezaji ukiwa kwenye soko la mitaji na kwenye migodi ya madini kunahitaji uwekezaji wa mtaji mkubwa na wamuda mrefu hivyo walikuja kuwaelimisha wananchi ili kutambua umuhimu wa hisa na hapa ni muhimu wananchi wakaungauna na hata kama mtu akiwa mmoja basi orbit wanaweza kukushika mkono .
Ameongeza kuwa Soko la mitaji Tanzania dhamira yake nikuona wanafadhiri kweli na likiwa na msaada mkubwa Kwa wachimbaji hasa Tanzania hivyo wanakwenda kujipanga kwani wameweza kujua umoja na vikundi vyao hivyo wanarudi ofisi ili kuweza kujipanga
Amesema mwaka huu ni wa sita maonyesho yanafanyika lakini bado mchimbaji anajiita mchimbaji mdogo hivyo lazima wakuwe na kwenda kwenye mchimbaji wa kati na mkubwa na Kampuni ziliizokuwa binafsi basi ziwe kampuni za umma .
Ameongeza kuwa kupitia Soko la mitaji wananchi kama wanakuwa wameshajiunga na kuwa na sifa wao wataendelea kuwapa mitaji ya muda mrefu kwani tayari watakuwa wameshakuwa na uwazi kwenye shughuli zao .
Hata hivyo ameishukuru Serikali kwa kuweka sera na kufanya maonyesho hayo yanafanyika na kilichobaki ni sekta binafsi sasa kufanya kazi ili kuweza kufikia malengo na kwa sasa wanapatikana Dar es Salaam maeneo posta Mpya.
No comments: