test

KAMPENI YA MAGIFTI DABO DABO YATUA MIKOANI NA ZANZIBAR

 



Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Ziwa Joseph Mutalemwa(wa pili kushoto) akimpatia zawadi ya fulana mteja wa mtandao wa Tigo Alicia Benedicto, wakati wa uzinduni wa promosheni ya Magifti Dabodabo iliyofanyika jijini Mwanza, Meneja wa tigo kanda ya Ziwa Kaskazini Robert Sanyagi(kushoto) na Meneja Biashara Tigopesa kanda ya Ziwa Christopher Charles wakishuhudia.

Mkurugenzi wa Tigo Zanzibar Aziz Ali( kushoto) akimpa Mkuu wa Wilaya ya Mjini(Znz), Rashid Simai Msaraka(katikati) zawadi ya fulana, wakati wa uzinduzi wa promosheni ya Magifti Dabodabo iliyofanyika visiwani Zanzibar, Meneja wa tigo kanda ya Unguja Visiwani, Mwajuma Senkanga(kulia)akishuhudia.

Na Mwandishi Wetu.

Ikumbukwe Tarehe 22 . Novemba . 2023 Kampuni ya Tigo ilitanganza uzinduzi wa kampeni yake mpya ya 'Magifti Dabo Dabo'. Kampeni ambayo imeandaliwa kwaajili ya kusherehekea wateja wao wote kwa malengo waliyoweza kuyakamilisha mwaka huu pamoja na kuwazawadia kwa uaminifu wao kwa kuwapatia wao na wapendwa wao zawadi zenye kusambaza upendo katika kipindi hiki cha sikukuu. 

Kampeni ya 'Magifti Dabo Dabo' itafanyika kwa siku 80, ikitumia msingi wa kampeni ya 'Cha Wote' ambayo ilikuwa inalenga katika kuhamasisha wateja kudumisha mtindo wa maisha ya kidigitali wakati huo huo ikiwa inawahamasisha kufanya tathmini ya malengo yao ya nusu mwaka.  Kampeni hiyo vile vile itawazawadia wateja zawadi za fedha taslimu kama hamasa ya kuendela kufuatilia malengo yao waliojiwekea pamoja na Magari Mawili mapya kabisa.

Wateja wataingia katika droo za zawadi za kila siku, kila wiki, mwezi pamoja na zawadi kuu kwa kila muamala unaofanywa kupitia Tigo Pesa na kwa bando lolote lililonunuliwa katika kipindi cha kampeni. Kadiri wateja wanavyofanya miamala mingi, ndivyo nafasi zao za kushinda zinavyoongezeka. Vile vile, wateja wa Tigo pia wana uhakika wa kujishindia bonasi za papo hapo za hadi dakika 35 (on-net) na SMS 25 wanaponunua vifurushi kuanzia Tshs 500 kupitia Tigo Pesa, Tigo Rusha, au muda wa maongezi. 
Ili kupata nafasi ya kujishindia Magifti Dabo Dabo na kusherehekea mafanikio yako pamoja na mpendwa wako piga *150*01# kwa miamala yako yote ukitumia Tigo Pesa na kununua vifurushi piga *147*00# au tembelea wakala wa Tigo Rusha aliye karibu nawe.

Kampeni hii itahusisha wateja wote Tanzania nzima Bara na Visiwani , kwa upande Mwingine wateja wa Tigo kutoka maeneo mbalimbali wamepongeza ujio wa Kampeni hii na kusema kuwa wapo tayari kufanya miamala kwa wingi ili kuibuka na ushindi.
KAMPENI YA MAGIFTI DABO DABO YATUA MIKOANI NA ZANZIBAR KAMPENI YA MAGIFTI DABO DABO YATUA MIKOANI NA ZANZIBAR Reviewed by Adery Masta on November 24, 2023 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.