Na Mwandishi Wetu.
Desemba , 18, 2023. Wafanyakazi wa Kampuni ya Tigo wametoa msaada wa Vyakula, Magodoro , Maji ya Kunywa , Mablanketi n.k kwa wahanga wa Katesh - Hanang Mkoani Manyara kutokana na maafa yaliyowakumba kutokana na Mvua kubwa zilizonyesha usiku wa kuamkia Desemba 03 , 2023 na kusababisha Sehemu ya Mlima Hanang kuporomoka na kusababisha kutiririka kwa tope katika maeneo ya Katesh na Gendabi na kupelekea Vifo pamoja na majeruhi.
Akikabidhi Vifaa hivyo Meneja wa Tigo, Kanda ya Kaskazini, Daniel Mainoya alieleza namna walivyoguswa na tukio hili na ndio maana walifikia maamuzi ya kutoa msaada kusaidia Waathirika hao.
" Wafanyakazi wa Tigo kama Watanzania wengine pia tuliguswa na maafa yaliyowakuta wenzetu , ambao baadhi walipoteza makazi yao na wengine kupoteza maisha , na ndio maana leo tumekuja kuungana na Watanzania wenzetu waliokubwa na maafa lakini pia na Rais Wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan ili kuwapa pole na kuwafariji "
Akitoa shukrani, Mhe, Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Bi. Janneth Mayanja alisema kuwa msaada uliotolewa na Tigo umegusa Waathirika kwa kiasi kikubwa sana hasa kwa kuzingatia mahitaji ya waathirika,haswa magodoro yatakayo weza kutatua swala la malazi. Aliendelea kwa kuhamasisha Taasisi nyingine na Watu binafsi kuiga mfano wa Tigo, kuja kujitolea kwa chochote watakachojaaliwa
WAFANYAKAZI WA TIGO WAWAKUMBUKA WALIOPATA MAAFA HANANG
Reviewed by Adery Masta
on
December 19, 2023
Rating:
No comments: