Na Mwandishi Wetu
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limeshiriki Maonesho ya GHANA TRADE EXPEDITION TO TANZANIA ( GHANA EXPO ) kama mwalikwa Maonesho ambayo yamelenga kufanya maonesho ya bidhaa mbalimbali chini ya Mwamvuli wa Africa Continental Free Trade Area ( AfCFTA ) TBS limetumia jukwaa hilo kutoa elimu kwa umma na wafanyabiashara pamoja na kujenga ufahamu wa majukumu ya taasisi hiyo kwa wageni kutoka nchini Ghana na wenyeji kuhusu utaratibu wa kuingiza bidhaa kutoka nje ya nchi.
Akizungumza na waandishi wa habari Januari 28, 2024 Afisa Masoko wa (TBS) Bi.Rhoda Mayugu amesema kuwa wametoa elimu kwa wageni kutoka nchi ya Ghana ambao wengi waliuliza kuhusu taratibu za uingizaji wa bidhaa nchini ili kukidhi matakwa ya viwango vya Tanzania.
"Elimu hiyo imetolewa na wengi wameishukuru TBS kwani hata walipoleta bidhaa zao kwa ajili ya maonesho walipata huduma nzuri pasipo usumbufu wowote". Amesema Bi. Rhoda
Aidha Bi. Rhoda amesema wenyeji waliohufika katika banda walielezwa kuhusu taratibu za kupata alama ya ubora ambayo itawasaidia kutanua wigo wa kukuza bidhaa zao katika Ukanda wa Afrika Mashariki.
Pamoja na hayo amesema wametoa elimu kwa watembeleaji waliotaka kujifunza kuhusu maelezo ya msingi yanayopatikana katika bidhaa ambazo zinakidhi Viwango kwa ajili ya matumizi ambapo ameainisha bidhaa kuwa bora inatakiwa iwe na alama ya ubora pamoja na kuonesha muda wa matumizi wa bidhaa hiyo.
Aidha Ametoa wito kwa wazalishaji na waagizaji wa bidhaa nchini kuzalisha bidhaa zinazokidhi matakwa ya viwango na salama kwa matumizi ya binadamu.
Vilevile amewaasa watumiaji wa bidhaa nchini kusoma maelezo yanayopatika katika vifungashio vya bidhaa ili kutambua muda wa matumizi na alama ya ubora wa bidhaa, ili kuwa na uhakika bidhaa wanazonunua kama zinafaa kwa matumizi.
Kwa Upande wake Afisa Ukaguzi (TBS), Bw. Adamu Mitumba amesema kuwa bidhaa za vyakula na vipodozi vinavyotoka nje ya nchi kabla ya kuingizwa nchini muagizaji anapaswa kupeleka sampuli ya bidhaa hiyo kupimwa na shirika hilo ili zipate kibali cha kuuzwa nchini.
"Bidhaa za vipodozi na vyakula zinahitaji ziwe na usajiri kutoka TBS, kama mfanyabiasha anasafirisha bidhaa hizo kutoka nje anatakiwa kuwasilisha sampuli ya bidhaa hizo ili kupimwa na TBS na kama zinakidhi Viwango ndipo ataruhusiwan kuleta hiyo shehena na kwa bidhaa ambazo si za chakula wanatakiwa kutumia mawakala wetu katika Kanda husika". Amesema Bw. Mitumba.
TBS WASHIRIKI MAONESHO YA GHANA EXPO 2024
Reviewed by Adery Masta
on
January 29, 2024
Rating:
No comments: