test

TIGO WAMZAWADIA MTEJA WAO MAGARI MAWILI

  Na Mwandishi Wetu.

                         

Cecilia Nduguru ameibuka Mshindi wa magari mawili aina ya TOYOTA URBAN CRUISER katika promosheni ya MAGIFTI DABO DABO ya Tigo ambayo imehitimishwa rasmi Leo Alhamis ya Februari , 15 , 2024 , ambapo Cecilia amemchagua Dada yake Jackline Nduguru ambaye naye amepewa moja ya Magari hayo mawili aliyoshindwa , ili kuleta maana halisi ya Jina la Promosheni Magifti DABO DABO ambapo ukishinda zawadi unamchagua na mwenzako wa kushinda naye.


Neema Nduguru ( dada wa Mshindi wa Magari Cecilia Nduguru ambaye hakuweza kufika eneo la tukio kwa sababu ya changamoto za maradhi ) ,  akikabidhiwa mfano wa funguo ya gari kwa niaba ya mshindi na Haji Manara pamoja na Hamisa Mobeto , Kulia ni Angelica Pesha Afisa Mkuu wa Tigo Pesa na Edwardina Mgendi - Mkurugenzi wa Masoko .


Jackline Nduguru , dada wa mshindi Cecilia Nduguru katika furaha ya kuliona gari lake alilozawadiwa na Tigo , baada ya kuchaguliwa kuwa mshindi Mwenza.

Akizungumza baada ya kukabidhi magari hayo mawili kwa wawakilishi wa Mshindi Afisa Mkuu Tigo Pesa - Angelica Pesha amewashukuru Watanzania kwa kushiriki katika kampeni hii ya Magifti DABO DABO ambayo imeacha Mamilionea ambapo wateja 92 wameshinda Fedha Taslimu Milioni 1 - Milioni 30 , Washindi 16 wamepelekwa Dubai na 12 Zanzibar ( safari zilizolipiwa kila kitu ) , Washindi 18 wameshinda TV , Subwoofer , Friji na Microwave na Mshindi wa Mwisho wa Kampeni ambaye amezawadiwa Magari Mapya mawili 0km .


Angelica Pesha ameongezea kuwa hawa washindi wameshinda kwasababu ya kufanya miamala mara kwa mara na Tigo Pesa , kama vile LUKU ,VIFURUSHI , MALIPO YA SERIKALI n.k , Aidha amewasihi wateja wa Tigo kuendelea kufanya miamala kwa wingi maana kuna mambo Mazuri yanakuja.

Nao kwa Upande wao Mabalozi wa Tigo HAJI MANARA na HAMISA MOBETO wameipongeza Kampuni ya Tigo kwa kurudisha kwa wateja wao kwa kutoa zawadi mbalimbali , suala ambalo limechangia kwa kiasi kikubwa kutimiza ndoto za wateja hasa wa hali ya chini .


TIGO WAMZAWADIA MTEJA WAO MAGARI MAWILI TIGO WAMZAWADIA MTEJA WAO MAGARI MAWILI Reviewed by Adery Masta on February 15, 2024 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.