Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo wa CCM Mkoa wa Manyara Comrade John Nzwalile ahimiza mshikamano na upendo baina ya viongozi na wanachama wa CCM Wilayani Simanjiro.
Akihutubia mkutano wa hadhara katika kata ya Lorbosiret kijijini Narakauo, Nzwalile amewataka wananchi na wanachama wa CCM kutokuwa na tabia ya kuchafuana maana ukimchafua mwana CCM unakichafua CCM
Aidha kabla ya mkutano huo wa hadhara, Nzwalile alitembelea baadhi ya mabalozi na kuteta na viongozi wa kimila maarufu kama Malaigwanani.
Imetolewa na Idara ya Siasa na Uenezi CCM Mkoa wa Manyara
Nzwalile ahimiza mshikamano baina ya viongozi na wana chama.
Reviewed by VISION MEDIATZBLOG
on
May 21, 2024
Rating:
No comments: