Rais Ebrahim Raisi, Waziri wa Mambo ya Nje Hossein Amir-Abdollahian na wengine kadhaa wamethibitishwa kufariki dunia katika ajali ya helikopta iliyotokea Jumapili kaskazini-magharibi mwa Iran, televisheni ya taifa imesema.
Majina ya baadhi ya waliofariki katika ajali hiyo ya helikopta kando na Rais wa Iran Ebrahim Raisi na Waziri wa Mambo ya Nje Hossein Amir-Abdollahian sasa yametolewa.
Shirika la habari la serikali IRNAA linasema kwamba ndani ya ndege hiyo pia alikuwemo Ayatollah Mohammad Ali Al-e Hashem, imamu wa Swala ya Ijumaa katika mji wa Tabriz, na Jenerali Malek Rahmati, gavana wa jimbo la Irani la Azabajani Mashariki.
Kamanda wa kitengo cha ulinzi wa rais, Sardar Seyed Mehdi Mousavi, pia aliuawa, pamoja na walinzi kadhaa na wafanyakazi wa helikopta ambao bado hawajatajwa.
Raisi alikuwa amepigiwa upatu kufika kilele cha utawala Iran
Alisimama karibu na kilele cha madaraka katika Jamhuri ya Kiislamu na alipendekezwa sana kwamba angefika hadi upe wa juu kuiongoza Iran
Kifo chake cha ghafla sasa kimemuacha na hali tofauti na matarajio .
Kuaga kwake katika ajali ya helikopta siku ya Jumapili kumezua uvumi unaokua juu ya nani hatimaye atachukua nafasi ya kiongozi mkuu Ayatollah Ali Khamenei mwenye umri wa miaka 85 ambaye afya yake mwenyewe imekuwa ikizungumziwa kwa muda mrefu.
Hatima mbaya ya rais wa Iran mwenye misimamo mikali haitarajiwi kuvuruga mwelekeo wa sera ya Iran au kuitikisa Jamhuri ya Kiislamu kwa njia yoyote ile.
Lakini itaweka katika mtihani mfumo ambapo watu wenye msimamo mkali wa kihafidhina sasa wanatawala matawi yote ya mamlaka, waliochaguliwa na ambao hawajachaguliwa.
Wapinzani wake watapongeza kuondoka kwa mwendesha mashtaka wa zamani anayeshutumiwa kwa jukumu la uamuzi katika mauaji makubwa ya wafungwa wa kisiasa katika miaka ya 1980 ambayo alikanusha; watatumaini mwisho wa utawala wake utaharakisha mwisho wa utawala huu.
Kwa wahafidhina watawala wa Iran, mazishi ya serikali yatakuwa tukio lililojaa hisia; pia itakuwa fursa ya kuanza kutuma ishara zao za mwendelezo.
Nafasi nyingine muhimu ambayo lazima ijazwe ni kiti kinachoshikiliwa na mhubiri huyu wa ngazi ya kati kwenye Bunge la Wataalamu, chombo kilichopewa mamlaka ya kuchagua kiongozi mkuu mpya, wakati mabadiliko hayo muhimu
Katiba ya Jamhuri ya Kiislamu ina suluhu la moja kwa moja kwa matukio ambapo rais hana uwezo wa kutekeleza majukumu yake kwa sababu ya ugonjwa, kifo au kushtakiwa na kuondolewa na bunge.
Inampa kazi makamu wa rais - katika hali hii, Mohammad Mokhber - kuendesha shughuli za nchi na kwa pamoja na wakuu wa bunge na mahakama kusimamia uchaguzi wa rais mpya ndani ya siku zisizozidi 50.
Hili lingetokea tu kwa kuthibitishwa kwa kiongozi mkuu, ambaye ndiye mwenye usemi wa mwisho katika masuala yote ya serikali nchini Iran.
Huku vyombo vya habari vya serikali vikithibitisha kwamba Rais Ebrahim Raisi amefariki, utawala nchini Iran utasonga mbele kufanya uchaguzi kama huo - ambao hauwezekani kukusanya maslahi zaidi miongoni mwa umma kuliko ule wa mwisho.
Mara ya mwisho, wapinzani wote wakubwa kwa Raisi walizuiwa kugombea, hivyo kumsafishia njia ya kuingia ofisini akiwa na idadi ndogo zaidi ya wapiga kura (takriban 30% ya wapiga kura wanaostahiki), huku wengi wakisusia walichokiona kama uchaguzi
.jpeg)