Ziara ya Kamati ya siasa ya Mkoa wa Manyara imeanza leo Mei 24,2024 Wilayani Kiteto, ikiongozwa na mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM Ndg. Peter Toima akiambatana na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Cuthbert Sendiga na wajumbe wengine.
Kamati hiyo imefanya ukaguzi wa Miradi yenye thamani ya Shilingi Bilioni 7.2 ikiwemo ujenzi wa daraja la mawe Mbeli, ujenzi wa chuo cha Veta, ujenzi wa jengo la Halmashauri, ujenzi wa majengo matatu (3) Hospitali ya Wilaya pamoja na ujenzi wa mradi wa Maji Esukuta ulioibuliwa na Wakala wa maji na usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) ambapo kwa sasa ujenzi umefikia asilimia 85 na unatekelezwa kwa kutumia Wataalamu wa Ndani (Force Account) huku ukitarajiwa kuhudumia zaidi ya wakazi 3,500.
Baada ya kufurahiahwa na teknolojia ya mawe katika ujenzi wa Madaraja, mwenyekiti wa CCM mkoa wa wa MANYARA, Ndg. Toima ameagiza miradi mingine ya madaraja mkoani manyara kutekelezwa kwa kutumia teknolojia hiyo ya mawe ili kuokoa gharama na pia kuwanufaisha wananchi wengi zaidi kutoka maeneo yanayozunguka miradi.
Aidha, RC. Sendiga ameeleza nia ya serikali ya kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo ili iweze kukamilishwa kwa wakati ikiwemo miradi ya Maji, elimu, afya n.k.
Pia amewataka wananchi kuongeza jitihada katika utunzaji wa vyanzo vya maji na mazingira.
No comments: