Agosti 05, 2024 : Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge ( kulia ) na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mhe. Petro Magoti ( pembeni yake kulia ) katika Banda la Tigo lililopo Maonesho ya Nane Nane Mkoani Morogoro , Aidha RC Kunenge ameipongeza Kampuni ya Tigo kwa kuwapa Wananchi urahisi wa kuzipata Huduma za Kidigitali na kubuni Kampeni mbalimbali zenye lengo la kuwanufaisha wateja wao.
Na Mwandishi Wetu.
Jana Agosti 05, 2024, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mhe. Petro Magoti walilitembelea Banda la Tigo lililopo Maonesho ya Nane Nane Mkoani Morogoro kwa lengo la kujionea Huduma mbalimbali zinazotolewa na Kampuni hiyo ambapo Kampuni ya Tigo imekuja na Fursa mbalimbali kwa Wadau wa Kilimo , Ufugaji na Uvuvi katika Maonesho haya , Fursa kama Vile Simu janja kwa Mkopo ambapo wanayo simu ya ZTE inayopatika kwa Tsh. 35000 na baada ya hapo mteja atalipa Tsh. 650 kwa siku , sambamba na hilo Kampuni inaendelea na Kampeni ya SAKO KWA BAKO ambapo wateja wataotembelea banda la Tigo watapata zawadi mbalimbali.Kwa taarifa zaidi Tembelea mitandao mbalimbali ya Kampuni ya Tigo.
RC KUNENGE ATEMBELEA BANDA LA TIGO MAONESHO YA NANE NANE MOROGORO
Reviewed by Adery Masta
on
August 06, 2024
Rating:
No comments: