test

TBS ELIMU KWA UMMA YATUA MKOANI KIGOMA

 Na Adery Masta.

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) linaendelea na Kampeni yake Ya kutoa Elimu Kwa Umma katika Ngazi za Wilaya ambapo hadi sasa Shirika hilo limetoa Elimu Kwa wananchi Wafanyabiashara na Wajasiriamali Wadogo Ndani ya Wilaya zaidi ya 94 nchi nzima na Lengo likiwa ni kuzifikia Wilaya Zote nchini.

Akizungumza  Jana Septemba ,13 Manispaa ya Ujiji Mkoani Kigoma Afisa Masoko Mwandamizi TBS Bi. Deborah Haule  amesema lengo la Shirika hilo ni kutoa Elimu Kwa Umma katika Ngazi za Wilaya zote.


" Kwa sasa TBS tumeamua kuwafikia Wajasiriamali ,Wafanyabiashara na wananchi katika Ngazi Za Wilaya ili kuwapatia utaratibu unaotakiwa kwa ajili ya kupata alama ya Ubora, kusajili majengo ya Biashara ya chakula na Vipodozi ili kuepuka Usumbufu unaoweza kujitokeza, umuhimu wa kununua bidhaa zenye ubora na namna ya kuwasiliana na TBS wapatapo changamoto yeyote. Elimu hii ya Umma ipo katika ngazi ya Wilaya na hadi sasa TBS imezifikia Wilaya zaidi ya 94".

Kampeni hiyo iliyofanyika Manispaa ya Kigoma Ujiji ilihusisha wataalam wa TBS walipopita katika maeneo ya mikusanyiko, maduka, na vikundi vya wajasiriamali, ambapo walitoa elimu kuhusu njia bora za kuhifadhi bidhaa na namna ya kutumia alama za viwango vya TBS ili kutambua ubora wa bidhaa hizo.



Wakizungumza kwa nyakati tofauti Bi. Farida Severino Mjasiriamali mdogo na Kondo Abdallah wamelipongeza Shirika la Viwango Tanzania ( TBS ) kwa Elimu waliyoamua kutoa kwa maana imewafumbua Mambo mengi kuhusu umuhimu wa Viwango katika bidhaa wanazozizalisha na kuzinunua.

Ikumbukwe , Kampeni hiyo pia ilifanyika katika wilaya za Kasulu, Buhigwe, na Uvinza mkoani Kigoma, na inatarajiwa kuuongeza ufahamu kuhusu viwango vya ubora na kanuni za TBS pamoja na kuimarisha ushirikiano kati ya TBS, wananchi na wafanyabiashara.
TBS ELIMU KWA UMMA YATUA MKOANI KIGOMA TBS ELIMU KWA UMMA YATUA MKOANI KIGOMA Reviewed by Adery Masta on September 14, 2024 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.