Afisa udhibiti ubora Kanda ya Magharibi (TBS) Bw. Hassan Hassan, akitoa elimu ya masuala ya udhibiti ubora kwa wananchi na wajasiriamali waliotembelea banda la TBS kwenye Maonesho ya tatu ya Wiki ya Mwanakatavi yanayoendelea katika viwanja vya Azimio Mpanda, Mkoani Katavi.
Na Adery Masta.
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limeendelea kutoa elimu ya masuala ya udhibiti ubora kwa wananchi na wajasiriamali katika Maonesho ya tatu ya Wiki ya Mwanakatavi yanayoendelea katika viwanja vya Azimio Mpanda Mkoani Katavi.
Maonyesho ya wiki ya mwanakatavi yanayofanyika siku Sita katika viwanja vya azimio yalizinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Mwanamvua Mrindoko , Tangu Oktoba 25 na yatahitimishwa Tarehe 31 mwaka huu ambayo yamebebwa na Kauli mbiu isemayo ,Chagua viongozi bora wa serikali za mitaa, imarisha uchumi kwa maendeleo endelevu.
TBS WATOA ELIMU KWA WANANCHI NA WAJASIRIAMALI , WIKI YA MWANAKATAVI
Reviewed by Adery Masta
on
October 31, 2024
Rating:
No comments: