SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limeendelea kutoa elimu ya viwango kwa wafanyabiashara,wenye viwanda na wananchi kwa ujumla katika Maonesho ya Wazalishaji wa Bidhaa za Viwanda (TIMEXPO) yanayofanyika katika viwanja vya sabasaba Jjijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 01,2024 Jijini Dar es salaam kwenye banda lao, Afisa Masoko Mwandamizi (TBS) Rhoda Mayugu amesema watumiaji wa bidhaa wanatakiwa kukagua bidhaa pale wanapohitaji kununua ikiwa kama zinakidhi matakwa ya sheria za viwango ili kuepuka gharama au hasara inayoweza kujitokeza kwa kutumia bidhaa ambazo hazijathibitishwa ubora wake.
TBS WAWAFIKIA WANANCHI MAONESHO YA TIMEXPO 2024
Reviewed by Adery Masta
on
October 01, 2024
Rating:
Reviewed by Adery Masta
on
October 01, 2024
Rating:




No comments: