test

DIT MBIONI KUFUNGUA KITUO UMAHIRI WA TEHAMA AFRIKA MASHARIKI

 Na Adery Masta.

Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) iko mbioni kufungua Kituo cha umahiri wa Tehama Kanda ya  Afrika Mashariki unaotekelezwa chini ya mradi wa EASTRIP ( East Africa Skills for Transformation and Regional Integration Project) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia ikitazamia kuboresha Elimu ya Ufundi na Ufundi Stadi katika nchi tatu za Afrika Mashariki (Tanzania, Kenya na Ethiopia) ili  kutekeleza kwa vitendo maono ya kuwa na Taifa lenye watu wenye ujuzi katika nyanja za Sayansi na Teknolojia na kuwa shindani katika ulimwengu wa leo. 

                            

Mratibu wa Mradi Kanda ya Afrika Mashariki, Cosam Joseph amesema mradi wa Estrip huo unalenga kuongoza udahili wa wanafunzi katika masomo ya ufundi na ufundi stadi pamoja na kuwezesha utengamano wa nchi shiriki katika masuala ya ufundi na ufundi stadi ili waweze kuendana na kasi ya mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia.

                         

"Dunia inayovyokwenda sasa hivi elimu ya ufundi ni elimu ambayo inathaminika kwa nchi ambazo zipo katika kuboresha uchumi wao hasa kuongeza uzalishaji kwenye viwanda. Ukiangalia kwa sasa  kuna pengo kubwa zaidi la watu wenye ujuzi wa kufanya uzalishaji kwenye viwanda "

Kosam ameyasema hayo mara baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo ya maabara za Tehama katika Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) Kampasi ya Dar es Salaam.

                          

Kwa Upande wake Mratibu wa kitaifa wa mradi wa Estrip Tanzania, Dkt Fredrick Salukele ambaye pia ni Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi kutoka Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, amesema kituo  cha umahiri wa Tehama DIT uliopewa jina la RAFIKI CENTER ni kiungo muhimu katika kutekeleza Sera mpya ya kitaifa ya Elimu inasisitiza masomo ya amali kuanzia ngazi ya Elimu ya Msingi mpaka Elimu ya juu.

"Mradi huu unalenga kuhimiza amali kama tunavyojua  sasa hivi dunia nzima inajiangalia zaidi kwenye masomo ya amali. Jengo hili la Rafiki center litatoa wabobezi katika Tehama, tunataka tuongeze nafasi za watanzania, nafasi za wenzetu kutoka Afrika Mashariki kuweza kuja kusoma masuala ya ujuzi wa  Teknolojia, kwenye Kilimo, kwenye viwanda ili tuweze kukua kwa pamoja"

                                    

Ili  kuhakikisha kituo cha umahiri wa Tehama Kanda ya Afrika Mashariki (DIT) kinaleta ufanisi uliokusudiwa, Mratibu wa Kituo Joseph Matiko amebainisha hatua za kimkakati zilizochukuliwa zikiwa ni mosi, kuhuisha mitaala 40 ikijumuisha mitaala 40  mitaala ya muda mrefu na muda mfupi. 

Hatua ya  pili ni kuwajengea uwezo wafanyakazi kupitia kozi za muda mfupi na muda mrefu, kozi Maalum kama ulinzi wa mtandaoni (cyber security)

                                  


"Tumewapeleka wafanyakazi nje ya nchi kujifunza utaalam kwa ajili ya kufundisha hapa. Pia tumewapeleka baadhi ya Walimu viwandani kwa mfano kwenye SGR,  kuna wafanyakazi wamekwenda kujifunza kule wakati wa set up system (wakati wa ufungaji mitambo) kwenye bwala la Mwl Nyerere. Kwahiyo wanajifunza ili waje kuwafundisha vijana wetu.


Pia amesema kuwa kupitia mradi huo DIT umeongeza idadi ya wanafunzi wa Tehama kufika 1500 ikiijumuisha wapya na wanaoendelea  ikilinganishwa na 800 wakati mradi unaanza huku kasi ya wanafunzi wa kike kujiunga na masomo ya Tehama ikiongezeka kufika 25% kutoka 10% hadi 15% kwa kipindi cha nyuma. 

                                      


Aidha, Matiko amesema Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) imeendelea kuwa kiungo muhimu kwa kuwaunganisha wanafunzi na viwanda ili kuwapa umahiri kupitia kauli mbiu ya "Teaching  Factory"


Tanzania inatekeleza mradi wa Estrip kwenye vyuo vitatu na jumla ya Kampasi 4 ambazo ni, Taasisi ya Teknolojia Dar es (DIT) Kampasi ya Dar es Salaam inayojenga kituo cha umahiri katika Tehama, DIT Kampasi ya Mwanza inayotekeleza umahiri katika utengemezaji wa bidhaa zinazotokana na ngozi. Taasisi nyingine ni Chuo cha usafirishaji cha Taifa (NIT) inayotekeleza umahiri wa usafirishaji wa ardhini na anga. Kituo cha mwisho ni Chuo cha ufundi stadi Arusha kinachotekeleza umahiri kwenye nishati jadilifu.

DIT MBIONI KUFUNGUA KITUO UMAHIRI WA TEHAMA AFRIKA MASHARIKI DIT MBIONI KUFUNGUA KITUO UMAHIRI WA TEHAMA AFRIKA MASHARIKI Reviewed by Adery Masta on November 15, 2024 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.