Wananchi Wilayani Mbulu Mkoani Manyara wameaswa kuwa mabalozi wa kupambana na maambukizi mapya ya Ukimwi
Rai hiyo imetolewa leo na Mbunge wa Jimbo la Mbulu Mjini Mhe. Zakaria Paul Isaay akiwa Mgeni Rasmi wakati wa maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani yaliyofanyika kijiji cha Kwermus Kata ya Nambis Halmashauri ya Mji wa Mbulu ambapo amewasihi wananchi kuacha tabia za kujihusisha na ngono zembe
"Tukiwa tunaadhimisha siku hii muhimu, niwasihi tu wananchi ni vema kila mmoja wetu akatambua umuhimu wa kupambana na maambukizi mapya ya VVU ili kuilinda jamii ya sasa na baadaye"
Maadhimisho ya UKIMWI yalikuwa na kauli mbiu isemayo "Chagua njia sahihi ya kutokomeza UKIMWI".
Wizara ya Afya Tanzania
Manyara Rs.
MBULU WAASWA KUWA MABALOZI WA KUPAMBANA NA UKIMWI
Reviewed by VISION MEDIATZBLOG
on
December 01, 2024
Rating:
No comments: