PDPC YA HIMIZA TAASISI ZA UMMA NA BINAFSI KUJISAJILI PDPC

test

 Watakiwa kujisajili Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi 



TUME ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) imezitaka taasisi mbalimbali kujisajili ili kuweza kuwahakikishia watanzania usalama wa taarifa zao binafsi wanazozitoa kwao nyakati za kupata huduma katika ofisi zao.



Wito umetolewa jana Jijini Mwanza wakati tume hiyo ilipokuwa ikizungumza na Waandishi Habari katika eneo hilo kuelezea msisitizo huo wa takwa la kisheria ambalo ni mhimu kwa sasa kutekelezwa na watoa huduma hiyo kabla ya muda wake kumalizika.


Mkurugenzi Mkuu wa PDPC Dk Emmanuel Mkilia alisema mwisho kusajiri kazi wanazofanya ni Aprili 30 na baada ya hapo hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wale watakaokuwa bado kusajiri huduma zao kwa taasisi hiyo.


Alisema sheria ya kujisajiri ni kuwezeaha ulinzi wa faragha za watanzania kwani katika dunia ya sasa ya mapinduzi makubwa ya teknolojia uhalifu wa kimtandao umekuwa ukijitokeza na kusababisha usumbufu kwa watu mbalimbali.



Wakati huo huo aliwaomba Waandishi Habari kuchakata Habari zao kwa kuzingatia maadili ya kazi zao huku wakitanguliza mbele jukumu la ulinzi wa taarifa binafsi za watu ili kutoingilia faragha zao binafsi.


Mkilia alisema nchi nzima zipo taasisi zaidi ya 140,000 lakini zilizosajiliwa ni 2000 wakati Mkoa wa Mwanza ukiwa na idadi ya taasisi chache zilizosajiriwa mpaka sasa.



Mkuu wa Uhusiano kwa Umma na Mawasiliano, Innocent Mungi alisema uzingatiaji wa taarifa zenye maslahi ya Umma ni mhimu kuzingatiwa na wachakata habari na kufanya anga ya mtandao kuwa salama.



Alisema taasisi zinaweza kujisajili kwa njia ya mtandao kwa kuingia kwenye Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi na kukamilisha mchakato wote huo na hivyo kuendesha shiughuli zao kwa misingi ya kisheria.


Mungi, alisema changamoto ya uzingatiaji wa utunzaji wa taarifa binafsi linafanywa na mataifa mengi kutokana na kuwepo kwa matukio ya uhalifu ambayo yanapelekea uingiliaji wa taarifa za watu.


Naye Mkurugenzi wa Usajili na Uzingatiaji PDPC, Mhandisi Stephen Wangwe alisema kuwa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu ipo haja zoezi hilo lisibabishe wagombea kudharalishwa kwa kutoa taarifa zao binafsi zenye maudhui mabaya.



Hivyo alitoa wito kwa watanzania kusajiri shiughuli zao hizo ili waweze kuaminiwa na wananchi kuwa hawatumii taarifa zao vibaya.

PDPC YA HIMIZA TAASISI ZA UMMA NA BINAFSI KUJISAJILI PDPC PDPC YA HIMIZA TAASISI ZA UMMA NA BINAFSI KUJISAJILI PDPC Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on March 22, 2025 Rating: 5

Post Comments

Powered by Blogger.