test

DCEA YATEKETEZA EKARI 157 ZA BANGI KONDOA

 


Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kondoa pamoja na wananchi wa Kata ya Haubi, wamefanikisha operesheni maalum ya kutokomeza kilimo haramu cha bangi katika maeneo ya Hifadhi ya Milima ya Haubi, wilayani Kondoa, mkoani Dodoma.


Akitoa taarifa kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Naibu Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano ya serikali DCEA Bw. Daniel Kasokola, amesema kwa kushirikiana na uongozi wa Wilaya ya Kondoa wamefanikiwa kuteketeza ekari 157 za mashamba ya bangi katika vijiji vya Ntomoko, Kinyasi na Haubi. Watuhumiwa saba wanashikiliwa kwa mahojiano, na pikipiki mbili zimekamatwa.



Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Fatuma Nyangasa, amesema serikali ya wilaya hiyo itaendelea kushirkiana kwa karibu na DCEA kuhakikisha bangi inatokomezwa. 



DCEA YATEKETEZA EKARI 157 ZA BANGI KONDOA DCEA YATEKETEZA EKARI 157 ZA BANGI KONDOA Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on May 23, 2025 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.