MNEC Qwihaya Aungana na Waamini Katika Ibada Takatifu Mafinga
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC), Ndg. Leornad Mahenda Qwihaya, ameungana na waumini wa Jimbo la Mafinga kushiriki Ibada Takatifu iliyoongozwa na Fr. Franchesco Msofu, Makamu wa Askofu wa Jimbo la Katoliki Mafinga.
Ibada hiyo imebeba ujumbe mzito wa kiroho uliosisitiza kuwa “Yatupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu” (Matendo 5:29), ambapo Ndg. Qwihaya ameonyesha mfano wa uongozi unaotanguliza imani, mshikamano na huduma kwa jamii.
Katika mahubiri yake, Makamu wa Askofu Fr. Franchesco Msofu aliwakumbusha waumini juu ya kusimama katika kweli na kumtumaini Mungu katikati ya changamoto za maisha, akisema:
“Imani ya kweli huonekana si wakati wa raha, bali pale unapobaki na Mungu hata unapojikuta peke yako.”
Baada ya ibada, MNEC Qwihaya ataongoza na kushiriki harambee maalumu ya uzinduzi wa albam ya kwaya ya Bikira Maria Mpalizwa Mbinguni inayoitwa “Natembea na Yesu”, akiunga mkono juhudi za waamini katika kukuza huduma ya nyimbo za injili na kuinua vipaji vya muziki wa kiroho.
Ushiriki wake ni ishara ya mshikamano na maono ya uongozi unaogusa maisha ya watu siyo tu kisiasa, bali pia kiimani na kijamii.

No comments: