Na Adery Masta.
Agosti 14 , 2025 , Mtandao namba moja nchini kwa utoaji wa Huduma za Kidigitali Yas , kupitia Kitengo chake Cha Utoaji wa Huduma za kifedha Kidigitali Mixx by Yas wamezindua Kampeni ya " KILA HATUA MIXX " , Kampeni Maalumu mahususi inayolenga kutoa suluhisho la utatuzi wa changamoto mbalimbali za kifedha ili kuhakikisha watanzania wote hususani watumiaji wa mtandao huo wanafikia malengo bila kikwazo za kifedha.
Kampeni hii inahamasisha watanzania kugeuza Kila hatua ya matumaini kuwa hatua ya maendeleo , ni hadithi ya mshikamano , uvumilivu na mafanikio, huku ikihamasisha zaidi kugeuza ndoto kuwa ukweli .
Akizungumza wakati wa Uzindizi wa Kampeni iyo Afisa Mtendaji Mkuu wa Mixx by Yas Bi. Angelica Pesha amesema
"Tangu safari yetu ya utoaji huduma za kibunifu na zinazozingatia mahitaji ya watanzania ianze mwaka 2010 mpaka leo tunajivunia mchango mkubwa na alama tunayoendelea kuiweka kwenye sekta ya fedha ikiwemo kuchochea Uchumi wa kidigitali.
Tunawezesha watanzania zaidi ya milioni 20 kufanya miamala mbalimbali ya kifedha ya takribani shilingi trilioni 6 kwa mwezi.
Kupitia fursa za uwakala wa huduma za kifedha tunatoa ajira zisizo za moja kwa moja kwa mawakala zaidi ya 200,000 nchi nzima.
Vile vile, mifumo yetu ya kifedha inawezesha wafanyabiasha zaidi ya 500,000 kupokea malipo ya bidhaa na huduma kidigitali.
Pia makampuni binafsi Pamoja na taasisi za umma zaidi 3,000 kukusanya na kufanya malipo ya mkupuo kwa wabia/suppliers na wafanyakazi wao.
Tumewezesha wateja zaidi ya milioni 6 kupata huduma za mikopo yenye thamani ya zaidi ya shilingi trilioni 1 hivyo kufanya malengo yao kutimia.
Kuchochea utamaduni wa kuweka akiba miongoni mwetu, tumewezesha watanzania kuweka akiba zenye thamani ya zaidi ya bilioni 600.
Haya yote yamewezeshwa na maono, mikakati na nia yetu ya dhati ya kuchochea ujumuishwaji wa kifedha kwa watanzania wote. Tunawashukuru wateja, washirika wetu na wadau mbali mbali wa sekta ya fedha na mawasiliano ambao wamekuwa nasi katika safari hii iliyojaa mafanikio na mchango chanya kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
Tunatambua kuwa safari hii bado ni ndefu kwani bado kuna watanzania ambao hawajafikiwa na huduma za kifedha mpaka sasa. Mixx tumejipanga kuendelea kubuni mikakati ambayo itachochea upatikanaji na utumiaji wa huduma za kifedha ikiwemo huduma za Mikopo, kuweka akiba, bima, uwekezaji n.k ili kuhakikisha kuwa tunakuwa na Tanzania ambayo kila mtu anafikia malengo yake bila kuwa na kikwazo cha kifedha ". Alimalizia Bi. Pesha

No comments: