"FICHUENI NA KUPNGA UKATILI DHDI YA WATOTO"- INSPEKTA FATUMA
Mkuu wa Dawati la Jinsia na Usalama wa Mtoto Wilaya ya Babati mkoani Manyara, Inspekta Fatuma Omary Silaa, ameitaka jamii kushirikiana na vyombo vya usalama katika kufichua na kupinga vitendo vya ukatili, Ili kuhakikisha watoto wanalelewa katika mazingira salama na kumaliza matukio ya ukatili wilayani humo.
Inspekta Fatuma ametoa wito huo baada ya kutembelea kituo cha watoto yatima cha Hosana na kukabidhi msaada wa vyakula mbalimbali kwa watoto wanaolelewa kituoni hapo.
Akizungumza katika ziara hiyo, Inspekta Fatuma amesema, “Natoa wito kwa jamii wote tushirikiane kwa pamoja kuvifichua na kuvipinga vitendo hivi vya ukatili. Tunatamani sana kwa wilaya yetu hii ya Babati kuyamaliza kabisa matukio haya.”
Kwa upande wake, mlezi wa kituo hicho, John Minja, ameishukuru Jeshi la Polisi kwa msaada huo na kuomba wadau wengine kujitokeza kusaidia watoto wenye uhitaji.
NI ZAIDI YA UPENDO: AFANDE FATUMA AFANYA JAMBO HILI KWA WATOTO YATIMA UTAPENDA
Reviewed by VISION MEDIATZBLOG
on
October 21, 2025
Rating:
Reviewed by VISION MEDIATZBLOG
on
October 21, 2025
Rating:


No comments: