test

POLISI WAWILI MBARONI KWA TUHUMA ZA MAUAJI BABATI

 Askari wawili wa jeshi la polisi wanashikiliwa kwa tuhuma za mauaji.



Jeshi la Polisi mkoani Manyara linawashikilia watu wanne, wakiwemo askari wawili wa jeshi hilo, kwa tuhuma za kuhusika na tukio la mauaji lililobainika Aprili 22, 2026 katika Kijiji cha Minjingu, Kata ya Nkaiti, Wilaya ya Babati.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Ahmed Makarani, uchunguzi wa kina unaendelea ili kubaini mazingira halisi ya tukio hilo.


Amesema kuwa hatua mbalimbali zinaendelea kuchukuliwa, ikiwa ni pamoja na kuwatafuta watu wengine wote wanaodaiwa kuhusika na tukio hilo.


Kamanda Makarani ameeleza kuwa ushahidi wa awali tayari umekusanywa na unasaidia kuelekeza mwelekeo wa uchunguzi huo. 


Ameongeza kuwa Jeshi la Polisi litaendelea kuhakikisha haki inatendeka kwa kuwachukulia hatua kali za kisheria wahusika wote mara baada ya uchunguzi kukamilika.


Aidha, ametoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na vyombo vya usalama kwa kutoa taarifa zitakazosaidia kukamilisha uchunguzi huo na kudumisha amani na utulivu katika eneo hilo.


POLISI WAWILI MBARONI KWA TUHUMA ZA MAUAJI BABATI POLISI WAWILI MBARONI KWA TUHUMA ZA MAUAJI BABATI Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on May 04, 2026 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.