test

PACOME APOTEZA MAISHA MWANZA BAADA YA KUWASHAMBULIA WAUMINI KWA PANGA KANISANI

 Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linafanya uchunguzi kufuatia tukio la kijana 

mmoja anayesadikiwa kuwa na ugonjwa wa akili aliyewashambulia waumini

wawili na kuwajeruhi kwa panga nje ya Kanisa la Katoliki wilayani Ukerewe 

wakati wa ibada,na yeye kupoteza maisha kutokana na majeraha aliyoyapata 

baada ya kushambuliwa na wananchi wenye hasira kali.




Leo,Aprili 5, 2026, majira ya saa 01:30 asubuhi, katika Parokia 

ya Kagunguli, Wilaya ya Ukerewe, wakati ibada ikiendelea, kijana 

aliyefahamika kwa jina la Renatus Silivester, miaka 38, (maarufu kama 

Pacome), mkazi wa kijiji hicho, aliingia katika kanisa hilo kupitia mlango wa 

upande wa kulia akiwa amebeba mfuko na kuelekea moja kwa moja 

madhabahuni, ndipo mwenyekiti wa parokia hiyo, Costantine Muumba Bituro, 

mwenye umri wa miaka 65, alipomshtukia kijana huyo kutokana na mienendo 

yake na kumtoa nje ya kanisa. Walipokuwa wakimhoji, kijana huyo alitoa 

upanga na kuwajeruhi watu wawili.

Kutokana na kitendo hicho, kundi la waumini na wananchi waliokuwa nje ya 

kanisa walimdhibiti mtuhumiwa kwa kumpiga kwa silaha za jadi na kumjeruhi 

sehemu mbalimbali za mwili wake. Mtuhumiwa alikimbizwa Hospitali ya Wilaya 

ya Ukerewe kwa matibabu kutokana na majeraha aliyoyapata, lakini alifariki 

dunia kabla ya kufikishwa hospitalini.

Majeruhi wa tukio hilo ni Costantine Muumba Bituro, miaka 65, mwenyekiti wa 

parokia, mkazi wa Kagunguli, aliyejeruhiwa kichwani na kwenye mikono yote, 

na Aloyce Christopher, miaka 57, mwanakwaya, aliyejeruhiwa mkono wa 

kushoto. Wote wamepelekwa Hospitali ya Kanda Bugando jijini Mwanza kwa 

matibabu zaidi na hali zao zinaendelea kuimarika. 

Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa kina kuhusiana na tukio hilo na 

kufuatilia hali ya majeruhi waliopelekwa hospitali.




PACOME APOTEZA MAISHA MWANZA BAADA YA KUWASHAMBULIA WAUMINI KWA PANGA KANISANI PACOME APOTEZA MAISHA MWANZA BAADA YA KUWASHAMBULIA WAUMINI KWA PANGA KANISANI Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on April 05, 2026 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.