test

NDINGA LA KISHUA KUTOLEWA , WAKISHUA MSIMU WA TATU

 >  Kampeni ya Wakishua kutoka Tigo yaendelea kuwazawadia wateja gari jipya,pesa taslim zenye thamani ya mamilioni na Vifaa  vya nyumbani kutoka Hisense

Dar es Salaam 23 Novemba 2022, Kampuni inayoongoza katika kuhakikisha Mtanzania anaishi maisha ya kidijitali, Tigo Tanzania, Leo imetangaza awamu ya tatu ya kampeni ya wakishua ya muda wa wiki (8) iliyopewa jina la “Ndinga la kishua” ,ambapo mteja anaye fanya miamala zaidi kupitia Tigo Pesa, atajishindia gari jipya kabisa aina ya Toyota Rush vile vile wateja wa Tigo kote nchini wanaofanya miamala mbali mbali watapata nafasi ya kujishindia zawadi za pesa taslimu kila siku na kila wiki zenye thamani ya mamilioni.

Promosheni hii inayoanaza leo na kutamatika tarehe 15 januari 2023 ni kilele cha kampeni ya wakishua iliyo zinduliwa septemba 2022, ambapo awamu ya kwanza ilishuhudia wateja wa Tigo wakitambulishwa kwa ushirikiano na Boomplay ,kisha  awamu ya pili kuzawadia wateja kifurushi cha vifaa vya nyumbani vya Hisense ,kulipia gharama zote za safari ya kwenda kutazama moja kwa moja mechi za kombe la dunia la mpira wa miguu nchini Qatar, dakika za papo hapo na bonsai za sms kwa wateja wote wanaonunua  kifurushi chochote kupitia Tigo Pesa


Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo , Afisa mkuu wa Tigo Pesa , Angelica Pesha alisema kuwa “Ni kweli tunaamini katika nguvu ya kujumuika pamoja kuwanufaisha watanzania hasa katika kipindi hiki cha siku kuu zinazokuja ,ndiyo maana tunayofuraha kutangaza promosheni ya ndinga la kishua ili kuwazawadia wateja wote wa Tigo Pesa  wakati huo huo kuwahimiza wateja wetu kufanya miamala kidijitali, mpango huu unathibitisha tena dhamira yetu ya kuendeleza ajenda ya ujumuishishwaji wa kifedha nchini na kuendelea kubadilisha maisha ya Watanzania.”



Pesha alisema “Msimu huu wa furaha , kupitia zawadi zetu za kila siku na za kila wiki tunaamini tutakuwa tunarudisha tabasamu ambazo zitaamsha kumbukumbu za watanzania wanapokaa na kujumuika na wapendwa wao , kwa promosheni hii tunawaomba wateja kutumia Tigo pesa kama njia salama ya kufanya miamala kutokana na urahisi wake na Amani ya akili anayoipata mteja na wafanya biashara”

Miamala ya Tigo Pesa ni pamoja na; Malipo ya bidhaa na huduma kupitia lipa kwa simu, malipo ya bili, malipo ya serikali, tuma pesa, pokea pesa, vuta pesa kutoka Bank, na kupokea pesa kutoka mahala popote duniani na nyinginezo nyingi zitamuwezesha mteja kuingia kwenye droo ya wiki na Mwezi  Pamoja na Droo kubwa ya kujishindia mamilioni ya Fedha, kifurushi cha vifaa vya nyumbani vya Hisense na mshindi mmoja atabahatika kuondoka na gari jipya kabisa aina ya Toyota Rush.



Ili kupata nafasi ya kujishindia zawadi za pesa taslimu (milioni 1 kila wiki, milioni 5 kwa Mwezi wa Disemba na zawadi kuu za pesa taslimu Milioni 10 na Milioni 20), Vifaa vya Nyumbani vya Hisense na gari jipya kabisa la Toyota Rush, tunawahimiza wateja kufanya miamala mingi iwezekanavyo kupitia Tigo Pesa app au piga *150*01#

NDINGA LA KISHUA KUTOLEWA , WAKISHUA MSIMU WA TATU NDINGA LA  KISHUA KUTOLEWA , WAKISHUA MSIMU WA TATU Reviewed by Adery Masta on November 23, 2022 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.