> Bidhaa za Hisense kuendelea kutolewa
Ijumaa ya Novemba 18, 2022, Kampuni inayoongoza Tanzania katika kuhakikisha mtanzania anaishi maisha ya kidijitali Tigo Tanzania, kupitia Promosheni yake ya WAKISHUA TWENZETU QATAR na Hisense kwa kushirikiana na kampuni ya HISENSE wameendelea kutoa tiketi za kwenda Qatar kushuhudia kombe la Dunia na zawadi ya Vyombo vya ndani kama vile Friji , Spika za mziki (SubWoofer), Smart Tv , pamoja na Microwave. Promosheni hiyo imeitimishwa rasmi ba safari ya kwanza ya kwenda QATAR kushuhudia kombe la dunia itaanza rasmi tarehe 29 mwezi huu.
Akizungumza wakati wa kuhitimisha promosheni iyo Afisa Mkuu wa Tigo Pesa Bi. Angelica Pesha amesema kuwa mchongo wa pili wa promosheni ya WAKISHUA umehitimishwa rasmi na kuongezea kuwa" Napenda kuwafahamisha kwamba tunaendelea na kampeni ya Wakishua maana kuna mchongo mwingine unakuja STAY TUNED , lakini pia niwakumbushe Kama wewe ni mteja wa Tigo unaweza kuwa Wakishua maana kuna zawadi nyingi zinaendelea kutolewa , kama ambavyo tumekua tukitoa zawadi mbalimbali ikiwemo tiketi za kwenda kuangalia kombe la dunia ambapo safari yetu ya kwanza itaanza tarehe 29 Mwezi huu kwahiyo endelea kufanya muamala unaweza kuibuka mshindi na kuwa WAKISHUA " Alimalizia.
Naye Meneja wa Wateja Maalum Tigo Pesa Bi. Mary Ruta amesema kuwa;
“Hawa ndio Washindi wetu wa mwisho kwenye promosheni, wamepatikana kwenye Droo ya wiki ya saba ya promotion yetu ya WAKISHUA TWENZETU QATAR na Hisense washindi hawa walifanya miamala mbalimbali ikiwemo kulipa bili, kufanya malipo ya serikali, kupokea pesa kutoka nchi za nje, Banki, mitandao mingine, Lipa kwa simu, kununua muda wa maongezi,kuchukua mikopo kupitia tigo pesa na huduma nyingine za Tigo pesa na baada ya kufanya hivyo waliingia kwenye droo na baadaye kuibuka washindi wa kampeni ya WAKISHUA TWENZETU QUATAR NA HISENSE, Kwa wateja wetu wa Tigo endeleeni kufanya miamala na Tigo pesa ili kujishindia zawadi mbalimbali maana mchongo mwingine unakuja , Hadi sasa tumepata washindi wote 50 watakao kwenda kushuhudia kombe la dunia mubashara (LIVE) Bado kampeni inaendelea na tutaendelea kutoa vifaa vya Hisense kwa wiki zinazofuata, lakini pia kaeni tayari kwa mchongo watatu wa wakishua ambapo zawadi zaidi zitatolewa.
Ikumbukwe kuwa washindi wetu wa Safari ya kwenda kushuhudia kombe la Dunia Qatar, safari yenu ya kwanza iliyolipiwa kila kitu itaanzia Airport Jijini Dar Es Salaam tarehe 29, hadi Dubai ambapo mtalala hapo na kesho yake safari ya Qatar kuangalia mechi na baadaye mtarudi Dubai kutalii na kuangalia mazingira kabla ya kurejea nchini " Alimalizia.
Naye Afisa masoko wa kampuni ya HISENSE Bwn.Joseph Mavura amesema kuwa kampuni ya Hisense
Inatoa punguzo la 20% katika maduka yao yote na huduma ya kusafirishiwa bidhaa utakazo nunua hadi nyumbani kwako bure (FREEE DELIVERY), hii ni kwa wateja wote watakao nunua bidhaa kutoka hisense na kulipia kwa njia ya Tigo pesa, pia tunaendelea kutoa vifaa vya Hisense kwa washindi wawili kila wiki
Alimalizia.
SHUHUDIA HAPA ILIVYOKUA MCHONGO WA PILI , WAKISHUA TWENZETU QATAR NA Hisense
Reviewed by Adery Masta
on
November 18, 2022
Rating:
No comments: