test

NDINGA LA KISHUA WIKI YA NNE , TAZAMA WASHINDI WOTE HAPA

  Na Mwandishi Wetu.

> Tigo Yawakabidhi Mamilioni na Vifaa vya Hisense Washindi wa Droo ya Nne ya Kampeni ya Ndinga la Kishua

Dar es Salaam 23 Desemba 2022: Kampuni ya mtandao wa simu za mkononi ya Tigo, leo imewakabidhi zawadi zao washindi wa droo ya nne ya Kampeni ya Ndinga la Kishua inayochezeshwa kwa watumiaji wa miamala ya Tigo Pesa.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Meneja wa Wateja Maalum wa Tigo Pesa, Mary Rutta amesema kampuni hiyo inafuraha kubwa kuendelea kuwazawadia wateja wake zawadi hizo na kuwataka wengine kuendelea kufanya miamala ya Tigo Pesa ili nao kujishindia zawadi mbalimbali kama vile pesa taslimu, vifaa vya Hisense au Ndinga jipya kabisa la Kishua aina ya Rush. Meneja huyo aliendelea kusema;

“Leo tuko kwenye tukio lingine la kutoa zawadi kwa washindi wetu wa droo ya nne katika kampeni ya Ndinga la Kishua na mpaka sasa tumeshapata washindi 32 wa pesa taslim waliojishindia milioni moja kila mmoja na tumeshapata washindi 8 waliojishindia vifaa vya kisasa kabisa kutoka kampuni ya Hisense ambavyo ni friji, Tv nchi 50, microwave, spika za muziki (sound bar).

“Tunawasihi wananchi waendelee kufanya miamala kupitia Tigo Pesa kwani wiki ijayo kuna droo nyingine ya wiki ambapo kama kawaida tutatafuta washindi wanane wa shilingi milioni moja moja na pia tutakuwa na washindi wanne wa mwisho wa mwezi watakaojishindia shilingi milioni tano kila mmoja.

“Unasubiri nini? Fanya miamala kwa kutumia Tigo Pesa kutuma pesa mitandao mingine, Tigo kwenda Tigo, kulipa bili, kutuma na kupokea pesa kutoka benki,  kutuma na kupokea pesa kutoka nje ya nchini, kukopa fedha kupitia huduma ya Bustisha au Nivushe, kufanya malipo serikali ili kujiweka katika nafasi ya kujishindia zawadi hizo.

“Fanya miamala ya Tigo Pesa ili uweze kushinda zawadi mwisho mwezi na ndiyo tunauaga mwaka na kuingia mwaka mpya kwa kishindo”. Alimaliza kusema meneja huyo.

Kwa upande Afisa Masoko wa Kampuni ya Hisense, Joseph Mavura watoaji wa vifaa vya Hisense amesema;

“Siku ya leo tunakwenda kutoa zawadi kwa washindi wetu wa kampeni ya Ndinga la Kishua, mamilioni ya pesa na vifaa vya Hisense.

“Wiki ijayo tunategemea kupata washindi wengine nane wa vifaa vya Hisense ambavyo ni Tv, friji, microwave na spika za muziki za kisasa (sound bar).

“Hivyo nawasihi wananchi wote kufanya miamala kwa kutumia Tigo Pesa ili waweze kujishindia vifaa hivi vya kisasa kabisa.


Naomba nimalizie kwa kuwatangazia wananchi wote punguzo vifaa vyetu la mpaka kufikia asilimia 20 kwenye maduka yetu yote hapa nchini.

Kwa upande wake mmoja wa washindi wa vifaa vya Hisense, Turumba Cloud akiwa na shangwe baada ya kukabidhiwa vifaa vyake alisema awali alihisi kama ni utani lakini kwakuwa alipigiwa na namba 100 ambayo hutumika kwa huduma kwa wateja na kuelezwa juu ya ushindi wake ndipo aliamini kidogo.

Baada kuelekezwa jinsi ya kwenda kuvichukua vifaa vyake na kuvikuta ofisini vikimsubiri ndipo amejionea faida ya kufanya miamala ya Tigo Pesa.

Miongoni mwa waliojishindia mamilioni ni Bi. Kashinde Fundikira ambaye naye alielezea furaha yake baada ya kujishindia kitita hicho na kuahidi kuendelea kufanya miamala ya Tigo Pesa ili aweze kujishindia Ndinga na Kishua mwisho wa mchezo.

NDINGA LA KISHUA WIKI YA NNE , TAZAMA WASHINDI WOTE HAPA NDINGA LA KISHUA WIKI YA NNE , TAZAMA WASHINDI WOTE HAPA Reviewed by Adery Masta on December 23, 2022 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.