Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, MHE. NAPE NNAUYE,akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mnara wa Tigo wilayani Kalambo,mkoani Rukwa,kupitia mradi wa UCSAF(Universal Communications Service Access Fund | Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote.) , JANUARI 8, 2023.
Baadhi ya Wananchi wa Kalambo,mkoani Rukwa wakicheza ngoma kuonesha kufurahia Uzinduzi wa Mnara wa Tigo katika eneo hilo.
Na Mwandishi Wetu.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mh. Nape Nnauye amezindua mnara wa mawasiliano katika eneo la Kalambo,mkoani Rukwa, uliojengwa kwa ushirikiano kati ya TigoZantel na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Tigo akiwemo Meneja wa Tigo kanda ya kusini Bw. Moses Busee pamoja na meneja wa Tigo Mkoa wa Rukwa Bw. Fransis Mwasamwene
Akizungumza wakati wa kuzindua mnara huo Waziri Nape amewapongeza Kampuni ya Tigo kwa Ushirikiano wao Mkubwa wa hali na mali kwa serikali katika kukuza TEHAMA Nchini ambapo Jumla ya minara mipya 46 imewekwa ikiwa lengo ni kuendelea kujumuisha wananchi wengi zaidi kwenye huduma za kifedha na za kidigitali. Kwa Upande Mwingine Mwakilishi kutoka Tigo amesema kuwa" Katika azma yetu ya kuhakikisha kwamba maeneo ya vijijini yanapata muunganisho wa mtandao, Tigo imekuwa ikishiriki katika kutuma maombi ya zabuni kutoka UCSAF tangu 2012. Tunashukuru kutambua kwamba katika mengi ya matukio hayo; serikali imekuwa sikivu vya kutosha, na kutupa fursa ya kuunga mkono sera yake ya kitaifa ya ICT ambayo inaonekana kupanua mawasiliano hadi vijijini. Leo tunakabidhi mnara huu,ambao tunaamini utaenda kuwahudumia watu Zaidi ya 3000,vile vile tuna mpango wa kufungua maduka yatakayo wahudumia wateja hawa wapya. Jumla sasa tutakuwa na minara 46 katika maeneo haya. Kwa kuhitimisha,naomba nichukue fursa hii kuwakaribisha wateja wetu wapya kwa huduma zetu zikiwemo Tigo Pesa,usajili wa laini za simu n.k "
WAZIRI NAPE AWAPONGEZA TIGO USHIRIKIANO WAO KATIKA KUKUZA TEHAMA , UZINDUZI WA MNARA RUKWA
Reviewed by Adery Masta
on
January 09, 2023
Rating:
No comments: