test

TIGO PESA WAMWAGA ZAWADI NA MAMILIONI YA PESA KWA MAWAKALA WAKE WAKISHUA.

Na Mwandishi Wetu

Kampuni namba moja nchini kwa utoaji wa huduma za Kidigitali Tigo Tanzania kupitia Huduma yake ya mfumo wa pesa Kidigitali Tigo Pesa , imetoa zawadi kwa Mawakala wake Wakubwa na Wadogo kutoka Tanzania Bara na Visiwani ikiwa ni sehemu ya kuhitimisha Kampeni yake iliyofanya vizuri ya WAKISHUA . 

Akizungumza Usiku wa tukio hili la kihistoria lililofanyika Jijini Dar Es Salaam Afisa Mkuu wa Tigo  Pesa Bi. Angelica Pesha amesema 

" Tukio la leo ni kwa ajili ya Mawakala wetu wakubwa na wadogo wanaotusaidia Kila siku ili kuweza kuwafikia wateja wetu na kuwapa huduma za Tigo Pesa , tumeona tujumuike nao kusheherekea mafanikio yetu ya mwaka 2022 sambamba na hayo tutatoa Zawadi Mbalimbali kwa mawakala wetu waliofanya vizuri , akiwemo Bi. Neema Swai atajipatia Milioni 15 akiwa kama wakala aliyefanya miamala mingi zaidi kwa Mwaka 2022 "

Wengine ni Said Khatibu Wakala kutoka Zanzibar ambaye ndiye mmoja wa wakala  aliyetoa huduma kwa mda mrefu zaidi na kwa mawanda mapana . 

Wakala Waziri Omary kutoka Kibaha ambaye ni wakala aliyefanya Vizuri katika kanda ya Pwani , na  Saba General Enterprises Limited ambaye huyu ni Wakala ambaye anafanya miamala kiufasaha yaani hana malalamiko ya wateja " . Alimalizia

Kwa upande wake Bi . Neema Swai Mshindi wa Milioni 15 kutoka TIGO PESA kama wakala aliyefanya miamala mingi zaidi , ameipongeza Kampuni ya Tigo kwa kuamua kuwakumbuka Mawakala wake kwa kuwazawadia zawadi mbalimbali na kuwakutanisha pamoja  .




TIGO PESA WAMWAGA ZAWADI NA MAMILIONI YA PESA KWA MAWAKALA WAKE WAKISHUA.  TIGO PESA WAMWAGA ZAWADI NA MAMILIONI YA PESA KWA MAWAKALA WAKE WAKISHUA. Reviewed by Adery Masta on February 13, 2023 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.