test

SAMSON ( MSHINDI WA WAKISHUA ) AKABIDHIWA RASMI GARI LAKE NYUMBANI KWAO KAHAMA

 


Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa Bwn. Joseph Mutalemwa ( Kulia )  akimkabidhi rasmi Gari aina ya TOYOTA RUSH Mshindi wa Promosheni ya NDINGA LA KISHUA na Tigo Pesa Bwn. Samson Daniel ( 25 ) Nyumbani kwao Kakola - Kahama.

Na Mwandishi Wetu.

Kampeni ya Ndinga la Kishua iliyoendeshwa na kuratibiwa na kampuni ya mawasiliano Tigo, leo imekabidhi rasmi gari aina ya Toyota Rush kwa mshindi wa Ndinga la Kishua  Bwn. Samson Daniel likiwa na vibali vyote  nyumbani kwao Kakola - Kahama .

Ikumbukwe wiki mbili zilizopita Mshindi Samson alikuja Dar Es Salaam kwa ajili ya kuliona gari lake alilojishindia na kufanya makabidhiano ya awali , ambapo uongozi wa Tigo Pesa ulimwambia kuwa atasafirishiwa gari lake hadi nyumbani kwao Kahama na kukabidhiwa Rasmi suala ambalo limetimia. Ikumbukwe kuwa kampeni ya “Ndinga la Kishua” ilianza toka mwaka jana mwezi Novemba ambapo wateja wa Tigo Pesa 70 waliibuka washindi wa pesa taslimu zaidi ya milioni 114 na mshindi 1 aliibuka mshindi wa gari jipya aina ya Toyota Rush lenye thamani ya shilingi milioni 78.



SAMSON ( MSHINDI WA WAKISHUA ) AKABIDHIWA RASMI GARI LAKE NYUMBANI KWAO KAHAMA SAMSON ( MSHINDI WA WAKISHUA ) AKABIDHIWA RASMI GARI LAKE NYUMBANI KWAO KAHAMA Reviewed by Adery Masta on February 12, 2023 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.