test

TIGO WAFUTURISHA MAWAKALA NA WATEJA WAKE WILAYA YA TEMEKE.

 Na Mwandishi Wetu.

Kampuni namba moja nchini katika utoaji wa huduma za Kidigitali Tigo , Leo Jumatatu ya April , 17 imefuturisha Mawakala na wateja wake katika wilaya ya Temeke , Iftari iliyoudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa dini ya kiislamu akiwemo Sheikh wa kata ya Temeke . 

Akizungumza baada ya Iftari hiyo Kaimu Afisa Mkuu wa Biashara Tigo Tanzania Bwn. Othman Madati amewashukuru wateja wa Tigo na Mawakala katika wilaya ya Temeke kwa kukubali mualiko huo na kwa kutumia huduma za mtandao wa Tigo .

" Tigo kama ilivyo kawaida yetu kurudisha kwa jamii , na kwakweli leo tunatoa shukran zetu za dhati kwa wateja na Mawakala wetu wa wilaya hii ya Temeke kwa kujumuika katika Iftar hii kwa maana kama ilivyo kawaida hasa katika Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan , Mwezi wa rehema na baraka uwajumuisha na kuwaunganisha watu pamoja , na ndio maana sisi kama Tigo tumeamua tukutane na Wateja Wetu si tu  Wilaya hii ya Temeke bali na maeneo Mengine bara na visiwani , Kwakweli tunashukuru sana na niwatakie mfungo Mwema "Alimalizia Bwn. Madati.

Naye Sheikh wa Kata ya Temeke ameipongeza Kampuni ya Tigo kwa tukio hili adhimu ambalo wameamua kulifanya katika Mwezi huu mtukufu wa Ramadhan.


TIGO WAFUTURISHA MAWAKALA NA WATEJA WAKE WILAYA YA TEMEKE.  TIGO WAFUTURISHA MAWAKALA NA WATEJA WAKE WILAYA YA TEMEKE. Reviewed by Adery Masta on April 18, 2023 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.