test

TAN WARRIORS SPORTS ACADEMY WAENDA ITALIA KUSHIRIKI MICHUANO YA SHIRIKISHO LA MICHEZO YA VYUO VIKUU

 


Na Mwandishi Wetu.

Tan Warriors Sports Academy inayojihusisha na kuwaendeleza Vijana katika mpira wa Miguu , Basketball , Riadha etc inayopatikana Mkoani Morogoro , Leo June , 20 , 2023 wameondoka Nchini kuelekea Italy kushiriki michuano ya Shirikisho la Michezo ya Vyuo Vikuu kwa mwaliko wa Chuo Kikuu cha Kamerino kilichopo nchini Italia.

Akizungumza katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere ( JNIA )Jijini Dar Es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Tan Warriors Sports Academy Bwn. Mainga Kalaita amesema kuwa Academy iyo imealikwa ili kushiriki Championship ya European Universities Sports Association Michuano ambayo imeanza tayari tangia June 17.

" Naomba nizishukuru Balozi zetu kwa kuendelea kutuongoza na kutupa ushirikiano mkubwa hadi tunafanikisha safari hii , Vijana hawa wameandaliwa vizuri na wanaenda kuiwakilisha nchi yetu katika michuano iyo , Lakini pia baada ya Michuano Vijana wetu watapata nafasi ya kutembelea Vilabu vikubwa duniani kama AC Milan , Juventus , Inter Milan na Fermo".
TAN WARRIORS SPORTS ACADEMY WAENDA ITALIA KUSHIRIKI MICHUANO YA SHIRIKISHO LA MICHEZO YA VYUO VIKUU TAN WARRIORS SPORTS ACADEMY WAENDA ITALIA KUSHIRIKI MICHUANO YA SHIRIKISHO LA MICHEZO YA VYUO VIKUU Reviewed by Adery Masta on June 20, 2023 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.