Na Fadhili Shabani-MANYARA.
Mtu mmoja amefariki dunia wilayani Bavati baada ya
kugongwa na gari katika eneo la ngarenaro kata ya bagara mkoani Manyara.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Manyara ACP
George Katabazi amesema tukio hilo limetokea eneo la ngarenaro kata ya bagara
kufuatia gari aina ya spasho lenye namba za usajili T460 AYZ kumgonga dereva
pikipiki nakufariki papo hapo huku chanzo ikiwa ni uzembe wa dereva wa gari.
amemtaja aliyefariki kuwa ni Apornary Herman ambae ni mtumishi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Babati vijijini mkoani Manyara.
Hata hivyo kamanda Katabazi ametoa rai
kwa watumiaji wote wa barabara kuzingatia sheria za usalama barabarani ili
kuepuka ajali zisizo za lazima.
sanjari na hayo Kamanda wa polisi mkoa wa
MANYARA ACP George Katabazi amewataka watumiaji wa vyombo vya moto mkoani
Manyara kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepukana na ajali hizo.
AJALI YAUA MTUMISHI WA HALMASHAURI YA BABATI DC NA KUJERUHI WAWILI.
Reviewed by VISIONMEDIA
on
July 12, 2023
Rating:
No comments: