test

MBIO ZA TIGO ZANTEL ZANZIBAR INTERNATIONAL MARATHON 2023 ZAZINDULIWA VISIWANI ZANZIBAR

 






Na Mwandishi Wetu

ZANZIBAR, 11 Julai 2023 — Mbia Maarufu za TigoZantel Zanzibar International Marathon (ZIM) zimezinduliwa kwa msimu wa tatu , ambazo zitazofanyika mwezi Oktoba 2023. Hatua hii inaashiria mabadiliko ya tarehe kutoka kipindi cha kawaida cha mwezi Julai kama ilivyozoweleka huko nyuma. Zanzibar International Marathon imezingatia kuinua uchumi na kuhamasisha biashara za ndani katika kipindi cha msimu wa chini (low season), na kufanya Zanzibar kuwa kitovu cha kuvutia wageni katika misimu yote ya mwaka. Katika marathoni hii, lengo kuu ni kusaidia watoto na vijana kupitia michezo, ili kuhamasisha na kuendeleza maisha yenye afya.

"Tunapenda pia kuwalinda watoto na vijana dhidi yamadawa ya kulevya na vitendo vya udhalilishaji. Tunaimani kwamba kupitia michezo, tunaweza kuwasaidia watoto wetu kufanikiwa katika njia mbalimbali na kujenga mustakabali bora kwa jamii yetu" 

Mdhamini wetu mkuu, Tigo Zantel, ameonyesha nia kubwa na yuko tayari kusaidia kwa asilimia mia moja (100%) kufanikisha malengo haya. Tunashukuru sana kwa msaada wao na kujitolea kwao katika kusaidia kampeni hii muhimu"

MENEJA MAUZO kutoka TIGO ZANTEL ZANZIBAR, Mohamed Waqid alisema “TigoZantel tumekuwa wadhamini wakuu wa mbio hizi za TigoZantel Zanzibar International Marathon toka mwaka jana - 2022 kwa kuwa tunaamini mbio hizi zinatupa jukwaa bora zaidi la kutangaza utalii wa Zanzibar, kukuza vipaji vya wanariadha, kuimarisha afya, na kuchangiakuchagiza uchumi wa bluu hapa visiwani Zanzibar.

"TigoZantel dhamira yetu ni kuendelea kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii inayotuzunguka kwa kuwekeza kwenye miradi/matukio yanayogusa hisia/maisha ya wateja wetu moja kwa moja kama mbio hizi za TigoZantel Zanzibar International Marathon.” Waqid aliongezea kwa kusema haya kuhusu ushiriki kwenye mbio hizo “Tunatambua kuwa hatuwezi kufanikiwa peke yetu bila kushirikiana na wadau wengine pamoja na serikali na hili tukio la leo ni moja kati ya mifano mingi ya namna bora ya kugusa jamii kwa kushirikiana na wadau. Tunapozindua msimu mpya wa TigoZantel Zanzibar International Marathon 2023, inayotarajiwa kufanyika tarehe 29 Oktoba 2023, wakimbiaji wote wa KM 5, 10 na 21 wataweza kujisajili na kulipia ushiriki wao kidigitali kupitia huduma yetu ya TigoPesa Lipa kwa Simu.”

Tunapenda pia kutoa shukrani za dhati kwa washirika wetu wa ndani, Rahisi Solution Ltd na Zanzibar Connections Co. Ltd (ComNet), ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kufanikisha azma hii. Mchango wao na ushirikiano wao wa karibu umekuwa kiungo muhimu katika kufanikisha malengo yetu. Zanzibar International Marathon inaahidi kulete mbio za kipekee, zenye kusisimua na dhamira ya kuhamasisha na kulinda watoto na vijana wetu. Tunawaalika waandishi wa habari, wageni wa heshima, na umma kushiriki nasi katika tukio hili la kusisimua, tukiazimisha umoja, kuendeleza

MBIO ZA TIGO ZANTEL ZANZIBAR INTERNATIONAL MARATHON 2023 ZAZINDULIWA VISIWANI ZANZIBAR MBIO ZA TIGO ZANTEL ZANZIBAR INTERNATIONAL MARATHON 2023 ZAZINDULIWA VISIWANI ZANZIBAR Reviewed by Adery Masta on July 12, 2023 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.