test

DIT KUFANYA UDAHILI WA WANAFUNZI KATIKA MAONESHO YA 18 YA ELIMU YA JUU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA

Na Mwandishi Wetu.


WAWEZA KUTAZAMA VIDEO HAPO JUU 


Taasisi ya Teknolojia Dar Es Salaam ( DIT ) inashiriki katika maonesho ya 18 ya Vyuo vya Elimu ya Juu Nchini yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar Es Salaam kuanzia Leo . Julai , 17, 2023 Hadi Julai , 22 , 2023 yakiwa na kauli Mbiu " KUKUZA UJUZI NCHINI KUPITIA ELIMU YA JUU , SAYANSI NA TEKNOLOJIA KWA UCHUMI IMARA NA SHINDANI ".
Akizungumza leo hii Afisa Uhusiano Mkuu DIT Bwn. Amani Kakana amesema , Maonesho haya yanafanyika ikiwa Dirisha la udahiri kwa duru ya kwanza limefunguliwa na litakua wazi mpaka Agosti 04. 2023 
" Naomba nichukue fursa hii kuwaalika wale wanafunzi wote wenye sifa ya kudahiliwa na Taasisi ya teknolojia Dar Es Salaam ( DIT ) kufika kwenye banda letu kwa ajili ya Udahili ili kujiunga nasi kwa mwaka wa masomo 2023/2024 pamoja na Udahili utaweza kujionea mambo mbalimbali ya Sayansi , Teknolojia na Ubunifu waliyofanywa na Taasisi yetu , Lakini waweza KUJISAJILI KATIKA MTANDAO KUPITIA https://admission.dit.ac.tz/admission/apply Karibuni sana  " amesema Bw. Kakana.

DIT KUFANYA UDAHILI WA WANAFUNZI KATIKA MAONESHO YA 18 YA ELIMU YA JUU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA DIT KUFANYA UDAHILI WA WANAFUNZI KATIKA MAONESHO YA 18 YA ELIMU YA JUU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA Reviewed by Adery Masta on July 17, 2023 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.